MCHEZAJI SIMBA KUELEKEA AFRIKA KUSINI
Baada ya kumaliza msimu akionekana kutokuwa fiti kwa asilimia huku akikosekana katika mechi nyingi za ligi msimu huu, taarifa zinaeleza kuwa beki wa Simba, Salim Mbonde, ataondoka nchini siku yoyote kuelekea Afrika Kusini.
Mbonde atasafirishwa na klabu yake kwa ajili ya uchunguzi wa kina juu ya majeraha ya goti lake ambalo limesababisha akosekane Uwanjani na kupelekea kushindwa kuhimili kiwango chake.
Beki huyo aliumia mwanzoni mwa msimu lakini alifanikiwa kutibiwa japo hajakaa muda mrefu ambapo baadaye alijitonesha tena na kushindwa kuwa sehemu ya mchezo kikosini.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar kabla ya msimu wa 2017/18 kuanza, Mbonde aliumia tena katika mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar uliopita na kupelekea kutolewa ikiwa ni dakika chache tu baada ya kuingia Uwanjani.
Kitendo cha kuumia dhidi ya Kagera kilimfanya Mbonde ashindwe kujizuia baada ya kuanza kutokwa na machozi akiugulia maumivu ya mguu wake.
Safi sana Mabingwa wetu Simba kwa kuwajali wachezaji wenu.
ReplyDeleteProtas-Iringa