May 23, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Haji Manara, umefunguka kwa kuwajibu wale wanaopinga mabadiliko ya klabu hiyo kuingia katika mfumo wa kisasa kiuendeshwaji.

Akizungumza kupitia kipindi cha michezo 'Radio EFM', Manara amesema si busara kwa wanachama hao baadhi wanaopinga mabadiliko kuzungumzia pembeni wakati katika mkutano mkuu hawakuhudhuria.

Manara amesema kuwa mabadiliko hayo hayajaamuliwa na watu wachache bali ni wanachama waliohudhuria mikutano yote ya klabu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa JK Nyerere waliridhia tangu ianze kufanyika.

Msemaji huyo ameeleza kushangazwa na watu wachache ambao wamekuwa wakiibuka mafichoni bila kujitokeza kwenye mkutano kupinga, badala ya kuhudhuria mikutano inayoitishwa ili kueleza hisia zao.

Kauli ya Manara imekuja kufuatia baadhi ya wanachama walioibuka na kupinga mabadiliko hayo wakidai kuwa katiba imefojiwa na hata mkutano wa dharura ulioitishwa juzi haukuwa halali bali batili.

Tayari Simba imekamilisha mchakato mzima baada ya kukutano katika mkutano uliofanyika Jumapili ya Mei 20 2018 na sasa katiba itapelekwa kwa Msajili wa serikali kusajiliwa na kitakachofuata ni kuandaa muundo tayari kwa mfumo kuanza.

5 COMMENTS:

  1. Hao wadharauliwe wanahisi tundu walizokuwa wakizitumia kiionyonya Simba sasa zimezibwa. Umati uliohudhuria mkurano wote wamewafiki je hao hawana aibu na vileile hawaoni haya wamekuwa kama vikoko vinabweka ovyo bila ya sababu na ukivisogelea hufyata mikia. Nawende kuungana na Akilikali ili waunge nguvu. Waungwana wakishangilia maendeleo ya timu kwao huwa msiba. Masikini roho zao. Wameshika katiba hairuhusu na huku serikali ikimpa hongera Mo. Hao washauruwe wafunguwe timu zao na kipato kitakuwa chao na wajiondoe Simba kabisa kabla hawajaparurwa

    ReplyDelete
  2. mabadiriko ni kitu kizuri, tatizo mabadiriko ya simba yameendeshwa kihuni toka mwanzom
    Kwanza mtu aliyetaka kuwekeza ndiye alitoa ofa ni kiasi gani anataka kuwekeza badala ya klabu kutoa ofa
    Pili kabla ya simba kuingia kwenye uwekezaji wanachama hakuna chombo cha kihasibu kilichofanya tathimini ya thamani ya klabu ya Simba kumbuka thamani ya Simba ni pamoja na idadi ya mashabiki walionano
    Tatu aliyetaka kuwekeza alianza kutoa pesa kabla hata mchakato haujaanza pia alishaingia makubaliano na viongozi wa Simba mfano Simba ilipoingia mkataba na Sport pesa mwekezaji alikuja juu kwa maana nyingine tayari mwekezaji alishaandaliwa mazingira hali hiyo ilizuia wawekezaji wengine kuingia kwenye mchakato wa kuwekeza simba si ajabu wangekuja na ofa nzuri zaidi
    Mwisho wanachama hawakuelimishwa juu ya mfumo wa hisa wanaoingia nini maana yake ndio maana Manara anashindwa kuwajibu wale wanaohoji kuwa mbona mwekezaji kapewa nguvu kubwa hata ya kutoa mwenyekiti Manara anajibu sababu mwekezaji ameweka pesa zake huku akiwa haelewi kuwa pale zinazohusika ni hisa bila kujali mwekezaji ameweka pesa kiasi gani
    wanasema wanachama wapya watalipia 400000 wamechukua vigezo vipi kuwachaji laki nne hivi wanachama wa Simba waliopo na thamani ya brandi , majengo, viwanja ukigawanya unapata thamani ya kila mwanachama ni laki nne

    ReplyDelete
  3. Mawazo ni mazuri na mimi nafikiri hakuna mabadiliko yanayoweza kuchangiwa bila ya kuwa na wapingaji. Kitu kikubwa hapa ni maendeleo na hatuwezi kuwaziba midomo watu wacha waseme ila mwishoni watajua lengo la klabu kufanya mabadiliko hayo. Kikubwa kwa sasa kila kitu kifanyike kwenye mikutano na wala si watu wachache waamue kama jinsi walivyofanya kupitisha kwenye mkutano mkubwa kama ule. Asiyetaka kuhudhuria mwacheni hatuwezi kuwalazimisha kila mmoja akubali mabadiliko ila kwenye mafanikio kila mmoja atakuja.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. Protas tatizo ni hao wanao ona tatizo wakiwa pembeni
    Makadirio yamefanywa kuwa na wanachama har 50000.Waliopo wamepewa hisa za laki 4 kila mmoja. Wapya wataotaka kuwa wanachama watalipa laki 4.Hicho ndio kiwango kilichokubaliwa na wanachama kwenye mkutano nasisitiza kwenye mkutano sio vijiwe vya kahawa.Ukiwa na maoni yapitishe kwenye njia halali kama alivyosema Waziri Mwakyembe. Zama za kupiga kelele pembeni na umahiri wa kuropoka kwenye vijiwe vya kahawa vimepitwa na wakati .Una la kusema njoo kwenye mkutano. Hoja zako zikishindwa na hoja za walio wengi basi ndio utaratibu wa demokrasia.

    ReplyDelete
  5. Mwana Simba damdam, ndo maana nimesema, waacheni wazungumze na kama kikao au mkutano umeamua na idadi ya wajumbe imeakidi hakuna haja ya kuwajibu kwa sababu hawana nafasi ya kuongelea kwenye vijiwe ama kahawa, wahudhurie kwenye vikao watoe hoja, watetee na kujadiliwa ndo hali halisi. Kubishana nao ni kupoteza muda wa maendeleo, tumechelewa kwa sababu ya kuendekeza watu haohao wenye malumbano bila hoja zenye mashiko. Waende na wakati, kipindi cha kupiga soga kimepitwa na wakati, SASA NI KAZI TU

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic