May 23, 2018


Na George Mganga

Kufuatia kushindwa kufanya hivi karibuni na licha ya kikosi cha Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa ligi uliopigwa jana Uwanja wa Taifa, mashabiki Yanga wameutaka uongozi wao kufanya mabadiliko.

Mapema baada ya mchezo dhidi ya Mbao kumalizika, baadhi ya wapenzi, mashabiki na wanachama walitoa maoni yao kuhusiana na mwenendo wa kikosi cha Yanga wakieleza ni vema Yanga ikaiga walichofanya Simba.

Wengi walieleza ni wakati mwafaka sasa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo ili kuepukana na kuyumba kwa uchumi, suala ambalo klabu inalipitia kwa sasa.

Mbali na hilo mashabiki hao wameeleza kuwa mfumo uliopo hivi sasa umesababisha Yanga kuwa na matatizo haya yanayoikumba hivi sasa haswa ukata wa fedha huku wakishauri ni muda sahihi kuondokana nao.

Wakati mashabiki hao wakitoa maoni hayo, watani zao wa jadi Simba tayari wameshakamilisha mchakato mzima na kilichosalia hivi sasa ni usajili wa katiba na uwezekano mkubwa wa mfumo huo kuanza kutumika upo kabla ya msimu ujao wa ligi kuanza.


2 COMMENTS:

  1. Sio kuiga tu bali ni lazima wampate muekezaji wa hakika na mwenye uwezo mkubwa wa kifedha. Hapa kuna tafauti kubwa baina ya Yanga na Simba. Mo kaipokea Simba wakati haina matatizo yoyote kwahivo kaipokea na na kuiendeleza kimali. Muekezi wa Yanga ataipokea timu wakati ina matatizo ya kila aina kwahivo jambo la kwanza ni kuiokoa timu kutokana na madeni ya mabilioni na baadae yanahitajiwa mabilioni mengine kuisuka upya Yanga hata iweze kusimama kwa miguu yake. Hii ni hali ya hakika iliyopo ndani ya timu na wala si yakubuni. Suala lilopo Jee atapatikana mwenye upendo na uwezo wa kulibeba jahazi hilo? Tunawatakia Yanga kila la heri?

    ReplyDelete
  2. Hapo ndipo wale walioipinga Yanga Yetu watakapoibuka upya!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic