May 22, 2018





Kampuni ya matangazo ya kidigitali ya StarTimes pamoja na SOS Children International zimesainiana mkataba wa makubaliano jijini Nairobi. Mkataba huo utafanya Kampuni hiyo na vituo vya SOS kushirikiana katika kusaidia familia na watoto wenye uhitaji, huku mkazo zaidi ukiwa ni kuwawezesha vijana kutizimiza malengo ya Kimaendeleo ambayo kama Umoja wa mataifa unavyohimiza.


Kupitia mkataba huo StarTimes itakuwa ikisaidia program na miradi mbalimbali katika nchi zaidi ya 10 barani Afrika ili kukuza nafasi za kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi kwa vijana ambao wako katika programu za vijiji vya SOS.


Hii itajumuisha mafunzo ya kiufundi na ujuzi pamoja na ushauri kwa vijana hawa huku wakipata nafasi ya Matangazo ya Kidigitali katika vituo vyao. Hii itawanufaisha vijana kuona fursa nyingi ambazo zinaambatana na matangazo ya kidigitali.


Akizungumza katika hafla ya kusainiana mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mahusiano Bw. William Masy alisema kwamba Kampuni hiyo ilifikia uamuzi huu wakati wa Mkutano mkuu wa YouthConnekt Afrika uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2017. Vijiji vya SOS vinatoa fursa kwa vijana kuingia moja kwa moja katika soko la ajira na kujitengenezea kesho yenye tija. 


“Kampuni ya StarTimes imejipanga kuhakikisha inawawezesha vijana kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kimaendeleo kupitia programu mbalimbali za mafunzo na malezi. Ndio maana ushirikiano huu ni zana kubwa katika kuelekea maendeleo ambayo kila mmoja wetu anayataka, vijana hawa watakuwa na ujuzi wa kutosha kukabiliana na changamoto ili kuendeleza jamii zao na vizazi vya baadaye,” alisema Masy 


Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SOS, Bi. Shubha Murthi alisema, “Ushirikiano kama huu ndio hufanya  kazi hii iwezekane. Tunaweza kufikia malengo ya kusaidia vijana kutimiza ndoto zao kupitia ushirikiano madhubuti wa Kampuni makini kama StarTimes. Matokeo ya kazi hii ni bora na yenye tija”. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic