May 5, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kukifanyia maboresho kikosi chake kutokana na kuonekana kwa mapungufu kadhaa haswa katika msimu huu wa ligi na mashindano ya kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano wa Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa hivi sasa wanajipanga kufanya usajili huo ili kukiongezea nguvu kikosi chao ambacho kinakabiliwa na mashindano ya kimataifa.

Yanga imekuwa inayumba kwenye safu ya ushambuliaji hivi sasa na eneo la kati kutokana na wachezaji wake ikiwemo Thaban Kamusoko, Donald Ngoma na Amis Tambwe kukumbwa na majeraha yaliyowafanya kukaa nje ya Uwanja wa muda mrefu.

Nyika amesema kuwa Mwalimu mpya tayari wanaye, huku akieleza kuwa masuala ya kufanya usajili si ya kukurupuka, hivyo watajipanga kufanya usajili huo wa wachezaji watatu muhimu.

"Ni kweli tuko kwenye mchakato wa kufanya usajili, lakini  bahati mbaya Mwalimu tuliyekuwa naye kwa muda mrefu ameshaondoka. Tunashukuru tumecheza mechi kubwa na Simba ambayo Mwalimu ameitumia kukisoma kikosi kuona wapi kina mapungufu, hivyo tumpe muda kabla ya kufanya usajili" amesema Nyika.

Kikosi cha Yanga kipo nchini Algeria hivi sasa ambapo kesho kitakuwa kinacheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

1 COMMENTS:

  1. Pesa za kusajili wachezaji wapya mnazo lakini za wachwzaji hamna

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic