Ukiangalia mwendo wa Real Madrid chini ya Kocha Zinedine Yazid Zidane unakuwa ni kama wa kusuasua hivi. Lakini imekuwa ikisonga taratibu na kufanya mambo makubwa.
Usiku wa kuamkia leo imeing'oa Bayern Munich na kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa tatu mfululizo.
Tayari imechukua mara mbili na kuweka rekodi ya kuwa timu iliyochukua ubingwa mara mbili mfululizo, hakuna nyingine iliyowahi kufanya hivyo.
Sasa inaongoza kwa kuchukua kombe hilo, lakini inataka kutafuta rekodi huko Kiev ya kulibeba kombe hilo moja kwa moja kwa mara ya kwanza na itakuwa ni dhidi ya AS Roma au Liverpool wanaokutana leo huko jijini Roma, Italia.
Zidane ameiongoza Madrid kuzifunga timu kubwa za ligi zote kubwa za Ulaya yaani England, Hispania, Ujerumani, Italia na Ufaransa na hasa katika hatua za mtoano na kuweza kutinga fainali na kuchukua kombe la UCL
Sasa yuko fainali, baada ya kuitoa timu ya Bundesliga, anasubiri timu kutoka Premier League au Serie A. Sijui atakuwa nani? Sijui atakeyekuja atamuweza kwa mwendo wake kama anasuasua, mwisho anakuwa mbabe. Tusubiri leo usiku.








0 COMMENTS:
Post a Comment