June 12, 2018


Kapteni wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, ametangazwa kuwa kocha mpya wa Nice inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa.

Vieira ambaye aliwahi pia kuzichezea Arsenal, Manchester City na Inter Milan ameteuliwa kuinoa Nice ikiwa ni baadaya ya kukosa nafasi ya kuitumikia Arsenal.

Awali kabla ya Unai Emery kutangazwa kuwa Kocha Mkuu Arsenal, kulikuwa na tetesi kubwa ingewezekana Vieira angeweza kurithi nafasi ya Wenger.

Vieira amejiunga na Nice akitokea New York City inayoshiriki Ligi Kuu Marekani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV