June 12, 2018



Kocha Pierre Lechantre naye ni kati ya waliopata tuzo katika Mo Awards, lakini ameaga Simba rasmi.

Lechantre alishukuru wakati benchi la ufundi likipewa tuzo maalum ya shukurani, naye aliwaongoza wasaidizi wake, Masoud Djuma na Mohammed Habib.
Baada ya kushukuru kwa tuzo hiyo, Lechantre alisema anawatakia Simba kila la kheri katika muendelezo mzuri wa mambo.

Ingawa hakusema moja kwa moja ilionyesha wazi kocha huyo amekamilisha ile ishu yake, kwamba anaondoka Simba.

Tayari uongozi wa Simba umeanza mchakato wa kusaka kocha na Selemani Matola kutoka Lipuli ni kati ya wanaopewa nafasi ya kuongeza nguvu.

Hata hivyo, kuna taarifa Simba imekuwa ikisaka kocha nje ya bara la Afrika kuchukua nafasi ya Mfaransa huyo ambaye huenda akaondoka kesho au keshokutwa kurejea kwao.


1 COMMENTS:

  1. Nimefurahia jinsi Uongozi wa Simba ulivyomchukulia Kocha huyo kwa kumuheshimu na kuonyesha uungwana hivyo hata pale alipoitelekeza timu kule Kenya. Huo ndio uongozi. Hata kama mnaachana na Kocha vizuri kuweka heshima sio kufukuzana na kuvunjiana heshima sio jambo jema. Hongereni Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic