June 19, 2018

Beki Juma Abdul ataendelea kubaki Yanga ikiwa ni kutokana na Azam FC kumsajili beki Nicholas Wadada kutoka Vipers ya Uganda.


Azam FC ilikuwa katika mazungumzo na Juma Abdul kwa zaidi ya wiki mbili lakini beki huyo wa kulia wa Yanga aliendelea kudai dau ambalo Azam FC waliona walikuwa hawawezi kutoa.


“Baada ya kuona hivyo, tuliamua kumsajili Wadada kuchukua nafasi yake. Sasa hatutakuwa na usajili mwingine kwa kuwa tunaona mahitaji yamekamilika.


“Limebaki suala la mshambuliaji, hili tutaendelea kulifanyia kazi tukiangalia kama kuna wachezaji wetu wanaweza kuondoka au mahitaji yakoje,” alisema mmoja wa wanaohusika na usajili.


Awali, Azam FC ilieleza ilikuwa njiani kumtangaza mchezaji kutoka kwa vigogo, yaani Yanga au Simba. Baadaye ikaelezwa alikuwa ni Juma Abdul ambaye alikuwa amependekezwa na Kocha Hans van Pluijm aliyetua Azam akitokea Singida United lakini kabla waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV