June 19, 2018



Mtu mmoja amefyatua risasi na kuua mtu mmoja huku ikielezwa amewajeruhi watu wengine wanne wakati akisherekea ushindi wa Sweden katika Kombe la Dunia.


Sweden iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Korea Kusini. Na shabiki huyo katikati ya mji wa Malmo nchini Sweden, alifyatua risasi hovyo na kusababisha kifo hicho. 

Baadhi ya watu walieleza kwamba mtu huyo alikuwa amelewa na alifyatua risasi ili kuonyesha furaha yake baada ya ushindi huo wa Sweden wakati timu kadhaa maarufu katika soka duniani kama Ujerumani, Brazil na Argentina hazikuwa zimepata ushindi.

Haijafahamika kama polisi wamemkamata mhusika kwani baada ya tukio hilo kulikuwa na taharuki na watu wakikimbia hovyo.

1 COMMENTS:

  1. Hii blog siku hadi siku inapoteza heshima nä hadhi yake ya kuwa blog inayoweza kuaminika.Tukio la Malmö hapa nchini Sweden ni tukio la kihalifu baina ya magenge ya uhalifu.Halihusiani kabisa na ushindi wa Jana wa Sweden dhidi ya Korea kusini.
    Kwa mujibu wa press conference ya polisi Leo sana 4 asubuhi waliuawa watu watatu wanaume wenye mpaka 19,27 na 29.Waliojeruhiwa pia ni watatu wenye umri wa mpaka 21,30 na 32.Kwa mujibu wa polisi huu ni muendelezo wa visasi baina ya magenge ya uhalifu.Na wote waliokufa nä kujeruhiwa ni wafuasi wa mojawapo ya magenge hayo.
    Kuandika habari kubwa kama hii bila ushahidi wa kutosha ni upotoshaji mkubwa hasa ukiihusisha na kombe la dunia.Naishi ja på Sweden nimeshangazwa sana na habari hii iliyoandikwa nä blog Hai.
    Ni muda muafaka sasa kuomba msamaha kwa wasomaji na kurekebisha habari hii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic