June 19, 2018




Kipa Aishi Manula hataichezea Simba katika michuano ya Kombe la Kagame.

Simba imeamua kumuweka Manula katika listi ya wachezaji wanaopumzishwa wakati wa michuano hiyo itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Manula ndiye kipa aliyedaka mechi nyingi zaidi kwa msimu uliopita kwa kuwa alishiriki michuano mingi akiwa na Simba.

Nafasi ya Manula itachukuliwa na Said Mohammed 'Nduda' ambaye alidaka mechi mbili tu za ligi kuu kutokana na kuandamwa na majeraha.

Pamoja na Manula, Simba imewapumzisha wachezaji wake zaidi akiwemo Haruna Niyonzima ambaye ni majeruhi.

3 COMMENTS:

  1. Simba mmefanya maamuzi mazuri kumpumzisha Manula na baadhi ya wachezaji nyota isipokuwa sajilini kipa mzuri kipindi hiki ili asaidiane na Nduda kwenye mashindano ya kagame.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic