June 8, 2018


Na George Mganga

Fainali ya Super Cup inayotarajiwa kupigwa Jumapili ya wiki hii mjini Nakuru, itakayowakutanisha miamba wa soka la Kenya na Tanzania, Gor Mahia na Simba imepewa uzito wa juu nchini humo.

Gor Mahia wametinga ambao wametinga hatua hiyo kwa kuindoa Singida United na Simba kuwaondosha Kakamega HomeBoyz FC wote wanapewa nafasi ya kutwaa taji hilo.

Ripoti mbalimbali kutoka Kenya zinaeleza kuwa kuelekea mechi hiyo timu zote zimepewa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 kutokana na kuwa mabingwa wa ligi za nchi zao kwa msimu wa 2017/18.

Simba wamefanikiwa kufika fainali bila kuruhusu nyavu zao kuguswa ndani ya dakika 90 na kupata ushindi kupitia changamoto ya mikwaju ya penati sawa na Gor Mahia ingawa wao hawajafanikiwa kufika hatua ya matuta katika michezo yao yote.

Uzito wa mechi hiyo unapewa uzito sawa kutokana na aina ya viwango ambavyo timu zote mbili zimeonesha licha ya Simba kucheza kiwango ambacho hakikuridhisha katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kariobang Sharks FC, tifauti na mchezo wa pili na Kakamega.

Katika mchezo huo Simba ilicheza zaidi eneo la kati na kwenye safu ya kiungo huku ikifeli kupandisha mashambulizi mbele, pengine inawezekana ni kutokana na aina ya mfumo ambao aliutumia Mfaransa, Pierre Lechantre.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic