JKU YAUNGANA NA YANGA KUYAAGA MASHINDANO YA SPORTPESA, YAPACHAPWA 3-0 NA GOR MAHIA
Na George Mganga
JKU nayo imeungana na Yanga kuyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup kufuatia kupoteza mchezo uliomalizika hivi punde kwa kufungwa mabao 3-0 na Gor Mahia FC kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru Kenya.
JKU inakuwa timu ya pili kutoka Tanzania kuondoshwa katika michuano baada ya Yanga kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kakamega HomeBoyz FC.
Mabao ya Gor Mahia yamefungwa na Odhiambo, Walusimbi na Meddy ambaye amepigilia msumari wa mwisho na kufanya ubao wa matokeo uwe 3-0.
Yanga na JKU zinatarajiwa kuanza safari ya kurejea nchini kesho huku Yanga wataanza maandalizi ya kibarua cha Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.
Simba na Singida United ndizo timu pekee zilizosalia hivi sasa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo yanaendelea huko Kenya.
Simba na Singida ndio mliobakia chonde chonde msituangushe watanzania.
ReplyDeleteVijana wa Msimbazi na Walima Alizeti kazeni buti kuhakiisha mnalinda heshima ya Tanzania.
ReplyDeleteProtas-Iringa