June 3, 2018



Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi ameamua kubwaga manyanga.


Mkemi ametangaza kuachia ngazi katika nafasi yake hiyo leo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, mara tu baada ya Yanga kufungwa mabao 3-1 na timu ya Kakamega Homeboyz.

Kakamega Homeboyz wameing’oa Yanga kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na kesho alfajiri itaondoka kurejea nyumbani Tanzania.

Kitendo hicho kinaonekana kumkwaza Mkemi ambaye amesema anatoa nafasi kwa mawazo mapya.

Juhudi za kumpata Mkemi hazijafanikiwa kwa kuwa simu yake imekuwa ikiita muda mrefu bila kupokelewa.

Rafiki mmoja wa Mkemi ameiambia SALEHJEMBE kwamba Mkemi alikerwa sana na kipigo hicho lakini wiki moja kabla amekuwa akizungumzia suala la kujiuzulu ingawa hakuwa amechukua hatua rasmi.

Juhudi nyingine zilifanyika ni kuupata uongozi wa Yanga mjini hapa na hasa Hussein Nyika ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na Mkemi, lakini naye simu yake haikupokelewa.

Hivi karibuni, kulikuwa na taarifa za kujiuzulu kwa Mkemi, lakini mwenyewe alipiga simu SALEHJEMBE na kulalamika kwamba hakuwa amejiuzulu kama ilivyoelezwa na kusema alizushiwa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic