KUELEKEA MKUTANO MKUU YANGA, AKILIMALI ATOA NENO HILI
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Yanga unaofanyika Jumapili ya leo katika ukumbi wa Police Officers Mess jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali ametoa neno lake.
Mzee huyo ambaye awali alionekana kupinga mabadiliko hayo amesema kuwa kwa sasa anayaunga mkono kwa asilimia zote.
Akilimali ameeleza kuwa mabadiliko Yanga kwa sasa hayakwepeki kutokana na timu yao ilipofikia hivi sasa mpaka kwa mwenendo ilionao kuwa si mzuri.
Kiongozi huyo amesema yeye hajawahi kupinga mabadiliko bali alikataa mfumo ambao alikuja nao Yusuph Manji hapo awali akitaka kukodisha timu na nembo jambo ambalo amefunguka kwa kueleza halikuwa sahihi kwake hata kidogo.
Ikumbukwe wakati Manji akiwa Mwenyekiti Yanga, alikuja na ombi la kutaka Yanga aikodishe akihitaji timu na nembo na baadhi ya wanachama ikiwemo Akilimali na wengine kuibuka na kupinga kwa nguvu suala hilo.
Mkutanoo Mkuu wa Yanga unatarajia kuanza leo majira ya saa 4 kamili za asubuhi ambapo Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mkwayembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
0 COMMENTS:
Post a Comment