June 11, 2018


Wakati Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiwapiga Mkwara wa kuwapa saa 48 watafakari kuhusiana na maamuzi yao ya kutuma barua wakitaka kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, amesisitiza hawatoshiriki.

Juzi Karia alisikika akisema kuwa Yanga wanapaswa kukaa na kujitafakari upya kutokana na maamuzi yao akieleza kuwa hayana mashiko, na akiwapa saa 48 pekee kutengua maamuzi yao.

Kwa mujibu wa Mkwasa, amesema kuwa kikosi chao kina wachezaji 7 pekee walio na mikataba huku wengine wote akieleza kuwa hawasaini na hivyo itakuwa ngumu kwao kushiriki mashindano hayo yanayotaraji kuanza Juni 28.

Mbali na wachezaji kukosa mikataba, Mkwasa amesema pia wachezaji wao wa kikosi cha pili wanashiriki mashindano ya Uhai CUP ambapo hawatoweza kutumika mara mbili.

"Hatuwezi kushiriki KAGAME sababu wachezaji wetu wapo likizo, wachezaji 7 tu ndiyo wana mikataba na wengine wote hawana. Wale wa kikosi cha pili wanashiriki Uhai CUP" alisema.

13 COMMENTS:

 1. suala kumbe ni mikataba siyo maandalizi ya michuano ya kimataifa! hali si shwari

  ReplyDelete
  Replies
  1. Maandalizi maana yake nini!? Ndo kuanzia kuhakikisha wachezaji wana mikataba, wamelipwa mishahara na marupurupu yao,wamefanya mzoezi nk. So unawezaje kupeleka timu kwenye mashindano wakati haiko kamili!?

   Delete
 2. Kweli Yanga hatukosi sababu. Kwa nini tunakuwa na maneno yasiyo ya kimpira? Tatizo ni mkataba au wachezaji kwenda likizo ama wacheaji wamegoma? Kueni wazi tatizo ni nini Yanga. Mbona Sportspesa wameshiriki,walikuwa na mkataba?

  Protas-Iringa

  ReplyDelete
  Replies
  1. Lazima mjue kuwa mikataba haiishi kama maji. Yanga ilienda sportspesa ikiwa na kikosi finyu cha wachezaji wachache waliokuwa wamebaki na mikataba. Ungekuwa unafuatilia ungejua hilo. Mbona kwenye mkutano viongozi wameelezea vizuri tu. Achananeni na habari za akina Salehe. Wanaandika ili wauze tu

   Delete
 3. Shirikisho watacheza hao saba pekee? Mkwasa anayumba sana

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ndo maana wamekwambia wanajipanga ili game za shirikisho wawe wameshamaliza matatizo yao.

   Delete
  2. Usiumize kichwa kumuelewesha chizi.timu inaenda kufanya nini kwa hali ilivyo yaani iwaridhishe watafuta mapato.wanatakiwa wajiulize inachezwa kila baada ya muda gani.na mwaka jana yamefanyika wapi na kama zipo sababu hayakufanyika.iweje yanga iwe ajabu kua na sababu

   Delete
 4. Lacuna town FAIR. Viongozi wa Yanga ndio wenye timu ndio wanaojua hali ya wachezaji ilivyo. Kama kungekuwa na tija kwa timu kushiriki asingepinga. Maadam wametoa sababu ya kutoshiriki itoshe kuamini wanachosema. Hivi kwanini TFF ilazimishe? Muda uliopo inatosha kuteua timu nyingine kushiriki.

  ReplyDelete
 5. @Winchislaus Rweyongeza usipoteze muda kuwajibu watu wanaojitoa ufahamu,maana hawajui wanachosema wala kuuliza wamebaki na ushabiki tu kama raisi wao wa TFF

  ReplyDelete
 6. We have to invest not only in financials but also in minds and mental.

  ReplyDelete
 7. I congratulate Mkwasa for his admission for the first tinme that Yanga is left only with seven players that means the remaining looking for a gap to snake out for future with security

  ReplyDelete
 8. Kweli uongo haudumu, ni hivi karibuni Yanga walizionya timu nyingine kutogusa wachezaji wao kwa vile bado wana mikataba,sasa Katibu wao kasahau anasema wachezaji hawana mikataba,duh ukisema uongo hutachelewa kusahau!!!!!

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV