June 11, 2018

Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameshangazwa na zaidi ya wanachama 1400 waliokutana kwenye Mkutano Mkuu wa klabu hiyo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Dar es Salaam na kuazimia kwa pamoja kuwa Yusuph Manji anapaswa kuendelea kuwa Mwenyekiti.

Katika Ajenda namba 5 iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kujadili barua ya aliyekuwa Mwenyekiti wao, Manji aliyoituma akitaka kujizulu, imepingwa na wanachama wote wa ujumla huku wakisema kuwa anafaa kuendelea kuwa Mwenyekiti.

Kutokana na maamuzi ya wanachama hao, Mzee Akilimali amekuja kivingine na kupinga maamuzi hayo akisema si jambo la kawaida kwa Manji kuendelea kuiongoza Yanga kwakuwa hakuna na timu kwa takribani mwaka mzima.

Mzee huyo ameeleza haiwezekani Manji akaendelea kuwa Mwenyekiti Yanga ilihali hajaweza hata kuwasili kwenye mkutano mkuu kuja kutoa hata sababu za kwanini aliamua kutuma barua hiyo.

"Haiwezekani mtu amekaa pembeni kwa takribani mwaka mzima halafu leo mnatoa maamuzi ya kutaka aendelee kuiongoza Yanga!! Kwanini asingeweza kuja hata kwenye mkutano akatoa sababu au hata kuomba radhi? Mimi sikubali" alisema.

Jumla ya wanachama wote 1400 wlaohudhuria mkutano huo wamepinga barua hiyo na wameridhia kuwa Manji ataendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.

14 COMMENTS:

  1. Waandishi mnakuza mambo kwa kuwapa platform na opportunities hawa wazee ambao hata hoja zao si za maendeleo ya mpira....mnaua soka la nchi kwa kuwapa fursa na platform za kuongea kwani hawa wanachangia kudumaza maendeleo ya mpira, lakini mnawapa platform ya hawa wazee kuwa vocal na hatimaye huleta chanzo cha migogoro sio lazima kila kitu cha Simba na Yanga kwenda kuwatafuta na kuwahoji hawa wazee....ifike wakati muache huu mtindo....ili maadui hawa wa maendeleo wasiweze kufurukuta....kinyume cha hapo watajiona kuwa mawazo yana maana sana lakini kwa uhalisia hayana maana. Hebu msiyakuze mambo nyinyi waandishi wa vyombo vya habari vya michezo

    ReplyDelete
  2. Vipi ataendelea na keshatangaza kujiuzulu hadi yakuwa hata hapo mkutanoni haypo. Ni aibu kujizalilisha hadi hiyo. Hapana sheria ya ya kumlazimisha kitu alichokwisha kukitema. Anajuwa kiachotakiwa ni hela yake na sio yeye binafsi. Hii ni sawa kumngojea maiti arejee katika uhai. Manji ni binaadamu na ana uamuzi wake na sio kuamuliwa ka maguvu. Mwacheni ajipumzikie kwa amani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama hujui in bora kukaa kimya, ndo maana baraza LA wazamini kabla ya kwenda mkutanoni waliongea naye ili awape maoni yake. Kwamba wewe una akiri kuliko akina Tarimba, Mkuchika, na wengine!?

      Delete
    2. Kama hujui in bora kukaa kimya, ndo maana baraza LA wazamini kabla ya kwenda mkutanoni waliongea naye ili awape maoni yake. Kwamba wewe una akiri kuliko akina Tarimba, Mkuchika, na wengine!?

      Delete
  3. hao wanachama 1400 wangechangia hata laki Yanga ingepata bilioni moja na laki nne ila kwa sababu akili zao zimekaa kitegemezi wanangojea Manji ndio aje awaendeshee timu halafu mnalalamika wahindi wanawanyanyasha kumbe mnanyanyaswa sababu ya kujidhalilisha wenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo ni story za abunuasi!! Soka lingekuwa hivyo nafikiri club zote nchi hii zingekuwa tajiri maana hakuna club ambayo haina wanachama 1400. Mpira in investment na si michango. Hakuna club duniani inaendeshwa kwa michango. Moira pesa. Huwezi kumchukia mtu kisa muhindi, umasikini wako ni akiri zako chafu tu. Ukiwa na hela huwezi mchukia mwenzio kwa rangi ama dini, huo ni uzwazwa.

      Delete
  4. Inaonekana hujapenda maamuzi, katika watu 1400 umeona hoja moja tu ya huyu mzee!? Nyie ndo mnaochangia kudidimiza soka letu. Angalau basi ungeangalia hata hoja,hoja ya kutokuwa na timu si hoja. Msipende kuwapa nafasi wapinga maendeleo, ndo maana rais Magufuri anapambana sana na watu kama hawa ambao Nazi yao ni kupinga kila kitu.

    ReplyDelete
  5. Sasa kama bado anaipenda timu yenu mbona akutokea kwenye mkutano kwanini mnamsemea mngeacha aseme mwenyewe kipindiiki nikigumu sana awezikukubali ictoshe yeye atakikua mwekezaji anataka kukodisha timu bure tena kwa miaka10 na serekali imeshatoa mwongozo %49 za mwekezaji %51 za wanachama sasaivi anapesa kama zamani kwakua alipata misukosuko mingi sana

    ReplyDelete
  6. Bado sijaona kosa la Manji, bado sijaona kosa la wanayanga 1400, nayaona makosa ya Mwandishi na nayaona makosa ya Mzee Akilidhiki.

    Kwann siyaoni makosa ya Manji ni baada ya kiongozi huyu kutangaza kujiuzuru kwa sababu alizozitoa lkn viongozi Wa matawi walikataa, kamati ya utendaji ilikataa, baraza la wadhamini lilikataa.

    Kilichokuwa kimebaki ni kurudi kwa wanachama kuwauliza wanasemaje?

    Wameulizwa Jana nao wamekataa, sasa hoja za wakosoaji zimesimamia kwenye kipengere kimoja tu.

    "Utajiri Wa Manji" kwamba mawazo yote ya Wanayanga fikra zao ni kufikiria utajiri Wa Manji na maendeleo ya Yanga.

    Hizi ni fikra zao na mawazo yao Mgando.kwann wasifikirie mbali zaidi na kushauri kwa njia chanya.

    Yanga imepitia ktk changamoto nyingi saana msimu huu ikiwemo hili gumu la kulipa mishahara ya wachezaji jiulize nani? Alijitokeza kusawazisha hilo.

    Mazungumzo yooote yanawezekana timu inaposhinda, iokoe timu kwenye shida utasikilizwa.

    Mzee Akilidhiki na hao wanaomuunga mkono jukumu kubwa ilikuwa ni kuiokoa timu kulipa kila inachodaiwa na kuweka sawa mazingira ya kusonga mbele.

    Wanayanga tu naamini Manji ni zaidi ya utajiri, huyu anaweza kutusimamia na kutuvusha kwenye Mipango thabiti ya maendeleo ya kudumu kuliko yeyote ktk mpira Wa nchi hii.

    Yote aliyoyapigia kelele na kuyasimamia kwa nguvu, ndo yanayoitafuna klabu kwa sasa.

    Pesa ndogo ya udhamini Wa Azam kwenye Vpl itapunguza mapato,kukataa pia udhamini Wa azam TV.

    Uuzaji Hovyo Wa jezi za Yanga na matumizi ya nembo, kupigania eneo la Jangwani klabu ijenge uwanja.

    Kupigania kitega uchumi kwenye jengo mitaa Wa mafia kariakoo.

    Hebu shaurini kwenye mawazo chanya, mshaurini na kumsisitiza Manji wanayanga wanaimani naye kubwa kuwavusha kwenye mafanikio kuliko MTU mwingine.

    Hii inatokana na dhiki walizopata huko nyuma mapambano mpaka kukaa sawa na sasa kutishia tena kurudi huko.

    Najua wapo wanaopendaturudi huko, najua wapo wanaonufaika na khali hiyo. Timu imara chini ya Manji itatuvusha.

    ReplyDelete
  7. Bado sijaona kosa la Manji, bado sijaona kosa la wanayanga 1400, nayaona makosa ya Mwandishi na nayaona makosa ya Mzee Akilidhiki.

  8. habari za huyu bwana akilimali huwa nazisoma katika blog hii tu, inanitia mashaka kuwa hii blog inatumika ndivyo sivyo katika kuimaliza Yanga. Hana jipya kila wakati anabadili kauli zake i mean kauli zake zinakinzana sana aisee

    ReplyDelete
  9. mwandish kilaza anapokutana na mzee pimbi matokeo yake ndio habar kama hizi

    ReplyDelete
  10. Kuna wakati wapenzi wa mchezo wa soka tunatakiwa kubadilika pia. Hivi kosa la Mwandishi hapa liko wapi? Kutimiza wajibu wake? Kama habari hii ingesema Mzee Ibrahim Akilimali anamuunga mkono Yusuf Manji Blog hii ingesifiwa sana, lakini kwasababu amekaririwa mtu anayemkosoa Manji linakuwa tatizo?
    Kwangu mimi Blog hii imetimiza wajibu wake kwa kuangalia maoni ya pande zote mbili kwa maana pia mawazo ya watu wengine.
    Hawa hao wanaokosoa kilichomo kwenye Blog hii wanaiamini na ndiyo maana wameweza kuisoma. Kweli Manji ni muhimu sana Yanga kwa wakati huu, lakini hii haina maana kwamba mawazo ya watu wengine yasipewe nafasi kwenye vyombo vya habari.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic