June 11, 2018


Wakati jana mkutano mkuu wa klabu ya Yanga ukifanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oyster Bay, Dar es Salaam, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Ibrahim Akilimali ametaja sababu za kutohudhuria.

Akilimali ambaye amekuwa akichukuliwa kama mpingaji mkuu wa mabadiliko ambayo yanatarajiwa kufanyika Yanga katika uendeshwaji wa klabu hiyo, amesema hofu kubwa iliyomfanya asiende ni kuepukana na kipigo.

Mzee huyo amesema kuwa Wanayanga wengi wamekuwa wakimtupia lawama wakisema kuwa amekuwa akipinga mabadiliko na wakidai amekuwa mtu wa kwanza pia kupinga Yusuf Manji kuendelea kuwa Mwenyekiti wa klabu.

Kutokana na lawama hizo, Akilimali aliona ni vema zaidi akabaki nyumbani kuliko kwenda kuambulia kichapo kwa wanachama walio na hasira kali na yeye.

Licha ya kushindwa kuhudhuria mkutanoni, Akilimali amepinga maamuzi ya wanachama wote waliokubaliana kuwa Manji aendelee kuwa mwenyekiti akisema si sahihi kwasababu alizozieleza kuwa hajawa na klabu kwa muda wa takribani mwaka mmoja.

5 COMMENTS:

  1. Tumechoka na habari zako za huyu mzee, kama unampenda sana mchukue ukanywe naye chai

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee hata haelewi nani ni mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za taasisi kama Yanga.Katibu mkuu ndiye mwenye majukumu ya kiutendaji ya kila siku akisaidiwa na wajumbe wa kamati ya utendaji,mwenyekiti ana majukumu machache sana kiasi kwamba anapata taarifa za kiutendaji za kila siku kupitia kwa katibu mkuu.Namshangaa kumsoma eti mwenyekiti alikuwa nje ya klabu kwa muda mrefu.Huku ni kukosa fadhila,shukrani na huruma kwa sababu hakuna asiyejua Yussuf Manji alikaa rumande muda gani na kisha alilazwa hospital muda gani,leo anatokea huyu ajuza anaongea utumbo mtupu uliojaa kinyesi bila hata chembe ya tafakari.Au baada ya lile fungu alilokuwa anapata la kamati ya utendaji ya wazee kukata sasa anatafuta namna ya kulirudisha kwa kutengeneza hoja zisizo na mashiko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watani wana kazi mwaka huu. Tengenezeni mfumo na muache kukomaa na mtu mmoja mmoja. Manji kaonesha kuwa hataki kuwa kiongozi wa Yanga, hakuna haja ya kumsujudia. Fanyeni hatua moja mbele kuliko tisa mbele halafu kumi nyuma.

      Delete
  3. Ikiwa anatakiwa au hatakiwi Kwa wakati huu Manji yuhoi anafikiri njia ya kujikwamuwa kutoka deni gumu la mabilioni linalo mnyima usingizi na juu ya yanga wasizidi kumsakama kwasababu yeye si mtoto wa kuamuliwa kimabavu anatazama maslahi yake kwanz

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic