June 11, 2018


Kikosi cha Simba kimerejea nchini usiku wa jana kikitoea, Nakuru, Kenya ambako kilienda kushiriki mashindano ya SportPesa Super CUP.

Kikosi hicho kimerudi ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wa fainali kw ajumla ya mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Afraha.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wamewahi kurejea kwa ajili ya halfa maalum ya uhawajwi wa tuzo za wachezaji wao unaofanyika leo kwenye Hotel ya Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zinazojulikana kama Mo Simba Awards, zitatolewa kwa viongozi, wachezaji, tawi na shabiki bora kwa msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa tuzo hizo, Mohammed Dewji 'Mo. amesema lengo kubwa la kuazishwa kwa tuzo hizo ni kutambua mchango wa walofanikisha kupata mafanikio makubwa ndani ya klabu ikiwemo ubingwa wa ligi kwa msimu uliomalizika.




3 COMMENTS:

  1. Nyie CIO mabingwa Ni msaada tu mliopewa spotpesa mmeshindwa hata kufunga goli hata LA kuotea

    ReplyDelete
  2. We value Mo's continuos efforts to show his great, sincere regards and admiration to Simba's players and out of that, came what we failed to win for half decade. All players and entire staff feel secured with joy for well wishers and a clear tremendous increase of fans. Keep it up Great Mo

    ReplyDelete
  3. hongereni simba kwa kuanzisha tuzo hizo zitawafanya wachezaji kujituma zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic