June 7, 2018


Taarifa zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, amekubali kurejea kurejea klabuni hapo endapo baadhi ya viongozi watakubali kuondoka.

Inalezwa Manji amekubali kiu ya wanachama na mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakihitaji uwepo wake, haswa baada ya klabu yao kuyumba kiuchumi wakati akiwa amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.

Mapema leo bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo chini ya George Mkuchika, ilikutana na Manji kwa ajili ya kumuomba aweze kurejea wakati klabu ikijiandaa kuelekea mkutano mkuu Juni 10 2018.

Taarifa zinasema baada ya mazungumzo, Manji amewataka baadhi ya viongozi waweze kujizulu kwanza ambao wanaenda kinyume na matakwa yake, kabla hajarejea klabuni hapo.

Manji ameomba iwe hivyo kutokana na baadhi ya viongozi ambao inaelezwa hajawataja majina kutaka waondoke kwanza ndipo aweze kurudi.

Mwenyekiti huyo wa zamani inaelezwa amefunguka kwa kusema viongozi hao anaotaka waondoke wamekuwa wakipinga uwekezaji pamoja na uwepo wake ndani ya Yanga huku akisema hafurahii namna klabu ilipofikia.

Kuelekea mkutano mkuu, jana viongozi wa matawi Yanga walikutana na kujadili mambo kadhaa kuelekea mkutano huo huku wakisisitiza kuwa kauli mbiu itakuwa ni Yusuph Manji na Mabadiliko.

6 COMMENTS:

  1. UWE UNAACHA KUVUJISHA SIRI ZA CLUB MBWA WEWE..KUJIFANYA MNAFKI KUFATILIA HABARI ZA YANGA KABLA WENYE YANGA YAO HAWAJASEMA, AU WEWE NDIO DISMAS TEN UMEKUWA MSEMAJI WA CLUB, KWENYE OFFICIAL SITE YA YANGA HII TAARIFA HAIPO WEWE UMEITOA WAPI KAZI KUHARIBU MIPANGO YA YANGA NDO HUWA UNAFURAHI..USISIKIE YANGA WAMETANGAZA MCHEZAJI ATA KABLA HAWAJAMSAINISHA WEWE UMBEA TU UMESHAWEKA HABARI MWISHO WA SIKU HEWA, JIFUNZE WEREDI WA KAZI YAKO, USIANDIKE KITU KABLA HAKIJADHIBITISHWA..

    ReplyDelete
  2. MMM kama ni kweli haya ngoja tuone masharti haya

    ReplyDelete
  3. Kwahivo katika kinyanganyiro cha kugombea uraisi, kweli atafuwa dafu mbele ya Mzee Akilimali na wafuasi wake ambaye kishatangaza kuutaka uraisi?

    ReplyDelete
  4. Haya Yanga, kufika ukweli ndo mafanikio?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  5. Msihangaike kwani huyo jamaa morali ya pale zamani hanayo tena. You may succeed to force the donkey to the river, but impossible to force him to drink the water while not feeling thirsty

    ReplyDelete
  6. Unafikiri kazitoa wapi kama sio dog wa Yanga kumpatia..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic