June 3, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kimeondoshwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Kakamega HomeBoys, mchezo uliopigwa mjini Nakuru, Kenya.

Kakamega wamejipatia mabao yao kupitia kwa Allan Wanga aliyefunga mawili huku moja likiwekwa kimiani na Opondo. Bao pekee la Yanga limewekwa kiminiani na Matheo Anthony kwa njia ya mpira wa faulo.

Matokeo hayo yanaibakiza Kakamega huku Yanga ikiyaaga rasmi mashindano na jumla ya timu nne kutoka Tanzania ambazo ni JKU, Singida United na Simba Sc zikisalia.

Yanga wamekosa nafasi ya kukupiga na Everton huko England, ambapo kama wangeweza kupata ubingwa wangepata fursa hiyo ya kucheza nao kwenye dimba la Goodison Park.

Muda mchache kuanzia sasa JKU kutoka Zanzibar itakuwa inakipiga na na mabingwa wa Ligi Kuu Kenya msimu uliomalizika, GorMahia FC.


5 COMMENTS:

  1. Bundi anaendelea kulia jangwani

    ReplyDelete
  2. Bora wangepelekwa hata Mbao kuliko hii aibu

    ReplyDelete
  3. Timu ya hovyo kabisa kuwahi kutokea, timu ambayo inalipwa millioni 950 kwa mwaka, nje na Voda, Azam tv, pamoja na viingilio lakini inalia njaa? shame

    ReplyDelete
  4. Sio Bundi anaendelea kulia Jangwani bali uwezekano wa Timu za Tanzania zote kupoteza katika mechi zao za kwanza upo mkubwa. Wakenya wapo serious katika haya mashindano. Sisi watanzania kama kawaida ni watu wa mzaha mzaha inapotokea nafasi ya maana ya kujitangaza hasa katika ngazi za kimataifa. Hata Simba kesho watafungwa na kutolewa kwani ile timu ni nzuri zaidi ya hii iliyoitoa Yanga. Kuondosha aibu ni Lazima wachezaji wa Simba wawe tayari kwa Jihadi ya kulinda heshima wa bingwa wa nchi.

    ReplyDelete
  5. Mambo yote yatakwenda sawa na kusahau uchungu wa kufungwa ovyo pale tu atapokamata Mzee Akili Mali kwani kaushutumu uongozi wa yanga kuwa ndio sababu ya kufungwa na anataka achukue hatam hata yanga iwe yanga sahihi ambayo kasema wakati huo simba iusahau ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic