June 8, 2018


Wakati vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara likiendelea, taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga wako kwenye mchakato wa kupata saini ya beki mkongwe wa Kagera Sugar, Juma Nyosso.

Nyosso aliyewahi kutamba na kikosi cha Simba miaka kadhaa nyuma ameingia katika rada za Yanga ili kuboresha safu yake ya ulinzi.

Yanga inaelezwa kuwa kwenye mazungumzo na Kagera pamoja na mchezaji ili kuweza kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ikiwa inatarajia kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC Julai 18 2018.

Mpaka sasa Yanga haijaweka wazi kwa asilimia 100 majina ya wachezaji waliowasajili tangu msimu wa 2017/18 umalizike, ingawa tetesi zinasema tayari imeshamalizana na mshambuliaji wake wa zamani, Mrisho Ngassa.

Ujio wa Nyosso katika kikosi cha Yanga unaweza kuongeza nguvu ambapo atakuwa anacheza sambamba na Kelvin Yondani ikiwa atasalia Yanga kwa kuwa uongozi una mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mwingine.

6 COMMENTS:

 1. Mhh Nyoso tena kweli Yanga tulipofikai kunatisha kunaitajika mkakakti wa haraka kuinusuru team

  ReplyDelete
 2. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 3. Sidhani kama kamati ya usajili ya Yanga wako makini hivi huyu mchezaji hata mtibwa hawako tayari kumsajili....udhaifu nwingine katika scouting ya important players....they need to change if they want to go far....usajili wa wachezaji wenye hadhi sio akina nyosso au ngasa!

  ReplyDelete
 4. Mwandishi wa habari hii anafanya ukuwadi kwa Nyosso akidhani viongozi wa Yanga wataingia mkenge.Uandishi wa kupika habari ndio unawafanya wasomaji wa blog hii kukosa imani na habari zenu.

  ReplyDelete
 5. Eeeh makubwaa...YANGA imeanza biashara ya wahenga...Ngassa,Nyoso na wasisahau kumrudisha Tegete, Dilunga

  ReplyDelete
 6. Hamna Yanga haina sababu ya kumsajili Juma Nyoso hana nidhamu na bangi waziwazi kwanini Yanga wajidhalilishe hivyo? Siamini

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV