Kampuni inayongoza katika michezo ya kubashiriki nchini, SportPesa inajivunia mafanikio iliyowapatia watanzania wengi walioshinda katika promosheni zao mbalimbali.
Tangu kampuni hiyo ianze biashara nchini, imeendesha promosheni mbalimbali ambazo washindi wake waliweza kubadili maisha yao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na Bajaji aina ya TVs King Deluxe, televisheni, simu za mkononi, jezi, tiketi za kuona mechi za klabu kubwa za Yanga na Simba na fedha taslimu.
Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema kuwa promosheni yao ya Shinda na SportPesa iliweza kubadili maisha ya Watanzania zaidi ya 100 ambapo ile ya Jiongeze na M-Pesa iliwafaidisha jumla ya watanzania zaidi ya 20.
Msuya alisema kuwa pia promosheni ya Amsha Amsha Ushinde na Airtel Money iliweza kuafaidisha washindi zaidi ya 50.
“Tumefarijika sana kuchangia ajira na kuondoa umaskini nchini kupitia promosheni mbalimbali za kampuni yetu, mpaka Watanzania wengi wamefanikiwa kujiongezea kipato, kuanzisha biashara kupitia promosheni zetu,” alisema Sabrina.
Alisema kuwa fursa kwa Watanzania ya kujiongeze kipato kupitia michezo yao bado ipo kwa kuendelea kubashiriki kwa kupitia kampuni yao.
Alifafanua kwa kusema kuwa wana michezo mbalimbali ya kubashiri ambayo ni, kubashiri kwa njia ya kawaida na masoko mingine 13. Kwa mujibu wa Msuya jackpot ya michezo yao inazidi kukuwa ambapo kwa sasa ni shilingi zaidi ya shilingi milioni 290 na kuwaomba Watanzania kujisajili kwa kutuma neno SOKA kwenda 15888 na baadaye Kukubali vigezo na Masharti yao kwa kutuma neno KUBALI.
Alisema kuwa unaweza kuweka fedha kupitia akaunti yao ya SportPesa kwa kutumia namba ya kampuni, 150888 na kumbukumbu namba 888 au neno SportPesa.
Alifafanua kuwa pia unaweza kucheza kwa njia ya meseji (sms) kwa kupiga USSD (*150*87#) na pia kwa njia ya mtandao (website) kupitia ‘app’; SPORTPESA APP









0 COMMENTS:
Post a Comment