Said Ndemla, Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga tayari wamejiunga na kikosi cha Simba nchini Uturuki.
Wachezaji hao wanne waliondoka leo alfajiri kwenda Uturuki na baada ya saa saba hewani walikuwa jijini Istanbul, Uturuki.
Usafiri wa gari ndogo kutoka Istanbul kwenda Kartepe kwa takribani saa tatu na nusu ndiyo uliwafikisha kambini na leo wamefanya mazoezi pamoja na wenzao.
Tayari kikosi cha Simba kilikuwa katika mji huo ulio milimani na wachezaji hao wameungana na wenzao.
Simba imeweka kambi katika milima ya Kartepe nchini Uturuki kujiandaa na msimu ujao wa 2018/19.








kuna kitu kwa Niyonzima, bado simuoni
ReplyDelete