July 14, 2018



Mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano ya Kombe la Kagame, Azam FC wamepongezwa kwa kazi nzuri ya kuendelea kuipa heshima Tanzania.

Mashabiki wapenda soka mitandaoni wameonyesha kuvutiwa na Azam FC na kuwapongeza kwa kazi nzuri iliyowawezesha kubeba ubingwa.

Azam FC waliifunga Simba kwa mabao 2-1 na kubeba Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfulilizo.

Baadhi ya mashabiki wameeleza Azam FC walivyoonyesha kiwango bora kuanzia mwanzoni mwa michuano hiyo hadi mwisho.

Wengne wamekuwa wakiitaka Azam FC kuendeleza kiwango hicho hadi katika Ligi Kuu Bara, msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. Moja ya timu dhaifu ni azam msimu ujao. Waendeleze makali kwenye ligi hiyo ndiyo message SAHIHI kwako. Manana Kama hao simba walikuwa wanatest tu mitambo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic