July 15, 2018


Baada ya kuwatambulisha kwa kuwarejesha wachezaji wake wa zamani, kiungo Deus Kaseke na mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa, uongozi wa Yanga umesema utatambulisha wengine siku yoyote kuanzia leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kunauwezekano mkubwa klabu ikatangaza wachezaji wengine wapya kabla ya kuelekea Nairobi Kenya kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Nyika ameeleza kwa sasa hakuna tena haja ya kuficha mambo bali ni hadharani tofauti na ilivyokuwa mwanzo ili kuondoa pia sintofahamu ya usajili unaofanywa na klabu hiyo kwa mashabiki wake.

"Tumewatambulisha wachezaji wetu wa zamani ambao wote wamesaini mkataba wa mwaka mmoja, na pengine kabla ya kuelekea tena Nairobi kucheza na Gor Mahia tunaweza kutambulisha wengine" alisema Nyika.

Yanga inatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Kenya kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo majira ya jioni kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza kwa CAF Confederation CUP dhidi ya Gor Mahia FC.

2 COMMENTS:

  1. SHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!! MBONA MNATAFUTA WA BEI CHEE!!!...TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WA MAANA KWA NAFASI ZA NAMBA 5, 6, 9, 7 NA 11.......NAANZA KUMWAMINI TARIMBA KUWA UONGOZI WA YANGA NI WA UBABAISHAJI NA WASANII TU, KUWADANGANYA WAPENZI WAO.....NA KAMA UONGOZI HUU UTAENDELEA NA MTINDO HUU....UBINGWA UTAKUWA WA SIMBA, AU AZAM.....SIDHANI KAMA WACHEZAJI DIZAINI HIZI WANAWEZA WAKASHINDANA NA TIMU KAMA SIMBA AU AZAM ZENYE VIKOSI KIPANA AMBAPO UNAWEZA UKAPATA HADI VIKOSI 2......TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU WATAKAOLETA USHINDANI....
    HUYO KOCHA ANAWALOSTISHA NA KUWASHAURI VIBAYA!! KAMA MNATEGEMEA KUSHINDANA NA KUTWAA UBINGWA KWA WACHEZAJI DIZAINI HIZI!!!!...YANGA INAKUWA KAMA LIPULI AU PRISON KWA USAJILI WA WACHEZAJI KAMA HAWA!

    ReplyDelete
  2. pana dalili ya maendeleo hapo. Yaani kusaini mwaka mmoja tu na wala sio miaka miwili kama ilivo kwa timu nyenginwzo halafu wanajigamba ati wameipiku Simba iliyosajili kila mchezaji walomtaka na huku wakisema wanapinga usajili wa wachezaji kumi wa kigeni. Ondokeni njiani msije kupigwa kikumbo na wenye nguvu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic