July 14, 2018


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemthibitisha Kidao Wilfred kuwa Katibu Mkuu wa TFF katika kikao kilichofanyika jana Julai 12,2018 Makao Makuu ya TFF Karume,Ilala.

Rais wa TFF Wallace Karia aliwasilisha suala la Kidao kwenye kikao hicho na Wajumbe kulipitisha na kuthibitisha rasmi Kidao katika nafasi hiyo.

Kamati ya utendaji pia imemthibitisha Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF.

Nafasi ya Madadi aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi iliyobaki wazi kamati ya utendaji imemthibitisha Kocha Oscar Mirambo kukaimu.

Katika hatua nyingine kikao hicho cha kamati ya Utendaji kimemuondoa Clement Sanga aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB) kwenye nafasi hiyo kwa kukosa sifa baada ya klabu ya Young Africans kuwasilisha barua iliyokuwa na maelezo ya kwamba Yusuph Manji ndio mwenyekiti wa klabu hiyo,Kamati ya Uchaguzi imeelekezwa kuandaa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo kamati ya utendaji imekubaliana kamati ya uchaguzi kuelezea mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokuwa wakati Sanga anaingia Bodi ya Ligi. 

Aidha kamati ya utendaji imepitisha kanuni mbalimbali ikiwemo kupitisha usajili wa idadi ya Wachezaji 10 wa Kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.

Wachezaji hao wa kigeni wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja kulingana na mahitaji ya klabu. 

Uamuzi huo umelenga katika kuboresha na kuleta ushindani zaidi kwenye Ligi pamoja na kupandisha viwango vya wachezaji wazawa. 

2 COMMENTS:

  1. Hii ndio bongo endeleen tu maana Rungu lenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani mambo yanayofanywa na TFF(tamka T chefuchefu)utadhani ni kundi la walevi wa komoni,wanafanya maamuzi kama vile shirikisho ni kwa ajili ya kikundi cha watu fulani.Ndo shida ya kuwapa nafasi watu wenye kubebwabebwa tu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic