COASTAL UNION YATHIBITISHA RASMI KUMSAINI KING KIBA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umethibitisha kuingia mkataba na Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Saleh Kiba maarufu kama King Kiba.
Coastal wamefikia maamuzi ya kumsainisha Kiba kwa kile walichokieleza kuwa ana kipaji cha mpira na wanaamini ataisaidia klabu hiyo.
Klabu hiyo imesema tayari jina la Kiba limeshawekwa kwenye mfumo wa mpya wa usajili unaotumika hivi sasa (TFF FIFA CONNECT) ambapo dirisha la usajili litafungwa leo majira ya saa 6 kamili usiku.
Taarifa za awali kutoka uongozi wa Coastal zilizema kuwa Kiba alikwenda mwenyewe kuomba nafasi ya kuichezea klabu hiyo kutokana na mapenzi yake ya kucheza mpira wa miguu.
Baada ya kuomba nafasi hiyo, uongozi wa Coastal Union ulianza mazungumzo ya kumalizana na Kiba na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao.








Ali Kiba ataipaisha sana Coastal Union..!
ReplyDeletePromo la kutosha hilo..!