July 26, 2018


Na George Mganga

Baada ya kushindwa kuondoka na kikosi Jumapili ya wiki iliyopita, wachezaji Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Said Ndemla wanaondoka alfajiri ya leo kuelekea Uturuki.

Wachezaji hao hawakufanikiwa kuondoka pamoja na wenzao kutokana na kuchelewa kwa viza hivyo ikabidi wapangiwe tarehe nyingine ya kusafiri.

Mbali na watatu hao tajwa hapo juu, kiungo mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar FC kwa miaka miwili, Hassan Dilunga, atakuwa katika msafara huo kuelekea Uturuki ambapo timu hiyo imewek kambi ya wiki mbili.

Dilunga alimalizana na Simba takribani wiki moja iliyopita japo uongozi haukutaka kuweka wazi juu ya usajili wake.

Baada ya kambi hiyo waliyoweka katika jiji la Instambul nchini kumalizika, kikosi cha Simba kinatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania Agosti 4 kwa ajili ya tamasha la Simba Day ambalo huazimishwa kila mwaka kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya watakaotumika msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic