July 26, 2018


Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha idadi ya wachezaji 10 wanaopaswa kusajiliwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Tenga, amefunguka na kutoa msimamo wake.

Tenga ameeleza kuwa inaweza kuwa uamuzi wa TFF unaweza kuwa sahihi ama si sahihi kutokana na ongezeko la wachezaji hao kutoka 7 mpaka 10.

Akizungumza mbele wa Waandishi wa Habari, Tenga amesema kama TFF wameamua kufanya hivyo wahakikishe kuwa uamuzi wao unaweza ukaleta faida ya kukuza soka la nyumbani.

Aidha ameeleza kuwa suala hilo vema likaangaliwa zaidi kwa jicho la tatu kwa kupitiwa upya kwa kina ili kuhakikisha kuwa maamuzi hayo yanaenda sawa na soka la Tanzania namna lilivyo.

Tenga ambaye aliwahi pia kuwa Rais wa TFF, ameliambia shirikisho kutokana na maamuzi yao wahakikishe wachezaji wa kigeni wanaoingia nchini wawe na ubora wa juu na si ilimradi tu wamesajiliwa.

Kiongozi huyo kutoka BMT amehoji juu ya suala hilo akieleza uamuzi huo pia uhakikishe Tanzania inapata faida kutokana na ongezeko hilo ili kulisongesha soka mbele badala ya kulirudisha nyuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic