July 25, 2018




Matarajio Jumapili wawakilishi wa Tanzania, Yanga watashuka uwanjani kupambana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa marudiano wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika utakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, kiungo Gor Mahia,  Francis Kahata ametamba kuwa baada ya kikosi chao kutumia vizuri mchezo wao wa nyumbani na kupata matokeo ya ushindi mbele ya wapinzani wao Yanga sasa wanakuja kupata matokeo mengine ya ushindi katika mchezo huo wa marudiano.

Gor Mahia, inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Kenya iliitandika Yanga mabao 4-0.

Kahata ambaye kwenye mchezo huo alitengeneza nafasi mbili za mabao amesema kuwa kazi yao waliyoifanya katika mchezo wa kwanza wanakuja tena kuifanya kwenye mchezo huo wa marudiano.

 “Katika mechi yetu ya nyumbani tulifanya kile ambacho tulikuwa tunakitaka hapa kwa kuchukua pointi zote tatu lakini hili kwetu tunaona bado halijatosha, tunataka pointi tatu nyingine Jumapili tutakapocheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa hapo Tanzania.

 “Tunajua tutakutana na upinzani wa mkubwa lakini ni matumaini yetu kuwa tutaibuka na ushindi kutokana na kikosi cha Yanga jinsi kilivyo sasa lakini pia hali ya mvurugano iliyopo klabuni hapo ambapo taarifa zao tumezipata huku kuwa mambo si mazuri, viongozi wao wameachia madaraka,” alisema Kahata.

5 COMMENTS:

  1. Nakumbuka kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika timu ya Simba iliwahi kufungwa na Mufulira Wanderers ya Zambia goli 4 -0 hapa Dar. Baada ya wiki 2 kwenye marudio kule Lusaka Zambia mbele ya Rais wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda , Simba iliwafunga wazambia goli 5-0 na kusonga mbele. Kwahiyo YANGA msikate tamaa piga hao Gormahia wekeni heshima ya nchi yetu. Mpira unadunda. INAWEZEKANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukwel unaongea ila siyo kwa yanga hii ya straika mkomola na buswita ata km mpira unadunda ila cyon sabab ya goh mahia kupoteza au kusare hii mechi naona bado nyepes xn KWA goh

      Delete
    2. Hakika Mpira unadunda..
      Lakini kwa hali ilivyo sasa..
      Huo Mpira utadundia zaidi upande mmoja!

      Delete
  2. Wapigeni tu hao vyura mana hamna namna tena

    ReplyDelete
  3. Hakuna beki wa kuwazuia washambuliaji wa Gor mahia ambao ni wahenga. Beki ninja, ni mzuri lakini sio kwa timu kama yanga. Kiufupi wachezaji wale niliowaona mechi ya kwanza Nairobi hawana uwezo wa kubadirisha chochote hata kama mpria unadunda. Kwanza mpira haudundi uwanja wa Taifa, ungedunda kama wangechezea uwanja wa Jamhuri Dodoma,ambao unapigiwa gwalide na kuwa mugumu kama mbuga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic