Ikionekana si katika hali isiyo ya kawaida, juzi Jumatatu wachezaji wa Mbeya City waligoma kufanya mazoezi huku sababu za kufanya hivyo zikiwa hazijawekwa wazi.
Mgomo huo wa wachezaji wa Mbeya City umekuja siku chache baada ya wale wa Yanga nao kugoma wakishinikiza kulipwa mishahara yao.
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurimo raia wa Burundi, alisema kuwa ameshangazwa na kitendo cha wachezaji wake kushindwa kufika mazoezini bila sababu ya msingi.
“Nilitarajia kuwaona wachezaji wote leo (juzi Jumatatu) wakiwa mazoezini, lakini wamekuja wachache wale wa majaribio tu, hili ni jambo la kushangaza kuona wachezaji wanashindwa kufika katika mazoezi na ikiwa tayari walishalipwa stahiki zao zote baada ya kukutana na viongozi. Jambo hili si zuri na nitalifikisha pia kwa uongozi wa klabu,” alisema Nswanzurimo.
Mbeya City ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, msimu ujao inatarajiwa kufungua kwa kucheza na Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.
SOURCE: CHAMPIONI







Duuuuh sasa mbeya city wanagoma ili iwaje tatzo wachezaj wa kibongo wanawai kulizika izi ndo tunaita kutojitambua na kutotambua kaz zao wanajal maslai kuliko kaz pia wafikilie MAISHA ya nje na mbeya city sasa wazoee kugoma tu ivo ivo adi kwa virabu vingne
ReplyDeleteUnajua lkn kilicho nyuma ya pazia au unaropoka tu
DeleteDuuuuh sasa mbeya city wanagoma ili iwaje tatzo wachezaj wa kibongo wanawai kulizika izi ndo tunaita kutojitambua na kutotambua kaz zao wanajal maslai kuliko kaz pia wafikilie MAISHA ya nje na mbeya city sasa wazoee kugoma tu ivo ivo adi kwa virabu vingne
ReplyDelete