July 6, 2018


Beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Vincent Kompany, amesema Brazil ina kikosi bora hivi sasa kwa kila mchezaji kuelekea mechi ya leo dhidi yao majira ya saa 3 usiku.

Kompany aliyekuwa majeruhi kabla ya kipute dhidi ya Japan ambacho alicheza, amefunguka na kueleza Brazi imebadilika na safu yao ya ulinzi imekubwa bora kwa sasa.

Kuelekea mechi ya leo hatua ya robo fainali, Kompany ameeleza kuwa watahakikisha wanacheza kiushirikiano zaidi ili kuweza kujitengenezea nafasi ya kupata matokeo.

Kompany anaamini wakicheza kama timu kwa ushirikiano tena kufa na kupona wana uhakika wa kupata matokeo na ikiwezekana kusonga mbele hatua inayofuata.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itakuwa inawakutanisha wachezaji wawili wa klabu moja wakiwa mataifa tofauti ambapo Kompany anayeichezea Manchester City lakini pia yupo Ubelgiji atacheza dhidi ya Gabrile Jesus ambaye pia anaichezea City na timu ya taifa akiwa Brazil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic