July 14, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano na beki kutoka Ivory Coast, Sergi Pascal Wawa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Wawa ambaye aliwahi kuichezea Azam FC miaka kadhaa nyuma ameingia kandarasi hiyo baada ya kuliridhisha benchi la ufundi la klabu ya Simba katika mashindano ya KAGAME.

Imeelezwa mkataba wa Wawa na Simba unamruhusu kuuvunja muda wowote endapo atahitaji kuondoka au pale klabu nyingine itakayojitokeza kuhitaji huduma yake.

Wawa anayecheza nafasi ya beki atakuwa pamoja na Erasto Nyoni eneo la ulinzi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic