BAADA YA KUMALIZANA NA TOTO, YANGA KUSHUSHA MASHINE HIZI MPYA MBILI
Baada ya kuchafua hewa juzi walipomsainisha kiungo fundi wa JKU ya Zanzibar, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika ameibuka na kutamba kuwa muda wowote kuanzia sasa watashusha mashine nyingine mbili hatari.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Yanga imemsajili Fei Toto baada ya kuzizidi ujanja Singida United na Simba iliyotenga kitita cha shilingi milioni 30 huku ikimpa mshahara wa milioni mbili kwa mwezi na gari la kutembelea.
Steringi mwenyewe wa hilo picha ni Nyika ambaye ameliambia Championi Jumamosi kuwa, ndiyo kwanza usajili umeanza baada ya kufanikiwa kumsajili Mohamed Issa ‘Banka’ Jaffary Mohamed na Deus Kaseke.
Nyika alisema, mashine hizo mbili watakazozitambulisha zote ni washambuliaji hatari ambao kazi yao ni kupachika mabao ambao majina ni siri kwa hivi sasa. Msikie Nyika; “Wote wanatoka nje ya nchi. Wachezaji hao wote wanacheza nafasi ya ushambuliaji namba 9 na 10 ambao tutawatangaza baada ya kukamirisha usajili wao na kikubwa tunataka kutengeneza kikosi imara kwa mahitaji ya kocha.”
“Kocha alipendekeza tusajili viungo kutokana na mahitaji yake ambayo tayari tumeyakamirisha hivi sasa tunaelekeza nguvu kwenye baadhi ya nafasi ikiwemo ya ushambuliaji na beki wa kati.” alisema.
Kaseke na Ngasa. Ndio hatari?
ReplyDelete