Na George Mganga
Katiba mpya ya klabu ya Simba inayoruhusu mfumo mpya uendeshaji imesajiliwa rasmi na Msajili wa wa Vyama vya Michezo nchini baada ya miezi kadhaa tangu ipitishwe.
Katiba hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wanachama pamoja na mashabiki wa Simba tayari imeshapitisha kila kitu tayari kuupokea mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu.
Katiba hiyo imekamilika ikiwa ni siku siku kadhaa zimesalia kwa Simba kuelekea kufanya uchaguzi wake mkuu baada ya viongozi waliopo madarakani hivi ssa kumaliza muda wao.
Baada ya usajili kukamilika, uongozi wa Simba umesema utakutana Julai kuteua Kamati ya Uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya Simba idara 37 ili kufanya utaratibu wa uchaguzi na kuwapata viongozi wapya watakaodumu kwa miaka minne.
Katiba hiyo ilifanyiwa maboresho hayo baada ya kumpata Mwekezaji wake, Bilionea kijana, Mohammed Dewji, aliyewekeza kwa asilimia 49 na 51 zikisalia kwa wanachama.








Kuna malalamiko kuwa pesa nyingi ya Yanga imetoweka. Ikiwa ni hivo ni kwanini ni viongozi wanaotuhimiwa kwa ubadhirifu na kufunguliwa kesi ni wa Simba tu ambao ama wapo baadhi kizuizini au nje ya nje inaonesha kama hofu ya sheria kuchukuwa mkondo au kuna mkono wa chinikwachini? Inajulikana kuwa sharia ni kama msumeno hukata tu penye ubavu
ReplyDeleteYanga ni ccm na ccm ni yanga..
ReplyDeleteUkifuatilia Waliopiga pesa za yanga lazima utathibitisha uwepo wa vigogo wa ccm..!!