July 28, 2018


Kesho Jumapili saa 1 usiku kwa saa za Tanzania Yanga itaikaribisha Gor Mahia katika mchezo wake wa raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mechi hii ni muhimu sana kwa wawakilishi wetu hawa wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, kwani ukiangalia katika kundi lao ambalo ni D wapo nafasi ya mwisho tena wakiwa na alama moja waliyoipata katika michezo mitatu.

Ni vyema wachezaji wakiingia uwanjani wakiwa wanafahamu kuwa wana deni kubwa ambalo ni lazima walilipe kwa kupata ushindi hapa nyumbani.

Ushindi kwenye mchezo huu unamaanisha kuwa sasa Yanga inaweza kuurejesha matumaini ya kuweza kusonga mbele au kumaliza hatua hiyo ikiwa kwenye nafasi nzuri.

Lakini pia Yanga inaweza kufanya vizuri ikiwa itapata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki watakaojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuwashangilia bila kujali matokeo yatakayotokea.

Uzalendo utakaoonyeshwa na mashabiki hao kwa Yanga utawashangaza wageni ambao wanaweza kubabaika na kupoteza mchezo na kama watakuta kuna kundi la Watanzania linawasapoti wao kwanza watatushangaa halafu itakuwa rahisi wao kutushinda.

Ni vyema mashabiki wakafahamu kuwa kuifanyia hujuma Yanga kwenye mchezo wa kesho ni sawa na kujiharibia sisi wenyewe kwani timu hiyo inawakilisha nchi na ndiyo ndugu zetu pekee waliobaki kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

5 COMMENTS:

  1. Hakuna kitu kama hicho palestina na israel hawawezi kuwa upande mmoja hata siku moja

    ReplyDelete
  2. Jee yanga itakuwa tayari kuiunga na kuipigia makofi simba, kwasababu Simba katika kombe la Kgame waliwashangilia Gor na ilipofungwa simba hawa jamaa walifurahi sana

    ReplyDelete
  3. Njoon tu muongeze mapato ht mkishangalia wakenya hakuna tatizo maana si kosa lenu ttz lipo wazi ........uzalendo c haiba yenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe unkown umewahi ishangilia Simba sc ikicheza na timu pinzani nje ya nchi?

      Delete
  4. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic