YANGA WAMTUMIA KASEKE KUIMALIZA GOR MAHIA
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amewaambia wapinzani wake Gor Mahia watarajie upinzani mkubwa katika mchezo huu wa marudiano utakaopigwa kesho Jumapili kutokana na mabadiliko ya kikosi chake ambacho ameongezeka Deus Kaseke na Anthony Matheo.
Wachezaji hao wanatarajiwa kuvaana na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inatarajia kuwatumia wachezaji hao baada ya kupata leseni kutoka Shirikisho la Soka la Afrika ‘Caf’ ya kuruhusu kuwatumia nyota hao walioongezwa katika usajili huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika.
Katika mazoezi ya mwisho ya juzi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, kocha alionekana kuwapanga kucheza pamoja Kaseke namba 10 na Matheo tisa katika vikosi viwili alivyovipanga katika mazoezi ya timu hiyo.
Katika mechi iliyopita ya Gor Mahia, kocha huyo aliwapanga kucheza washambuliaji wa katikati ni Juma Mahadhi na Pius Buswita katika kikosi cha kwanza kilichofungwa mabao 4-0.
Pia, katika mechi hiyo wataongezeka viungo wawili ambao hawakuwepo katika mchezo uliopita na Gor Mahia uliochezwa Nairobi, Kenya ambao ni Raphael Daudi na Juma Makapu ambao wote walikuwa na adhabu ya kadi mbili za njano ambao mechi hii wataanza kucheza pamoja.
Zahera alisema: “Maandalizi yanakwenda vizuri kuelekea mechi na Gor Mahia, kikubwa tutaingia uwanjani kwa ajili ya kazi moja pekee ya kupata ushindi ili kurejesha matumaini ya kusonga mbele katika michuano hii.
“Licha ya maandalizi yetu kuwa ya kusuasua yakienda sambamba na wachezaji kudai mishahara na fedha za usajili kwa wale wachezaji ambao mikataba yao imemalizika.
“Juzi, Alhamisi kabla ya mazoezi ya asubuhi tuliyofanya Uwanja wa Taifa nilizungumza na wachezaji na kuwarudisha katika morali nzuri kwa kuwaambia kila kitu kitakaa hivi karibuni kikubwa tupambane tupate matokeo mazuri.
“Nafurahia kuona kikosi changu kikiwa na mabadiliko makubwa katika mechi hii kwa kuongezeka Kaseke, Matheo majina yao yalitumwa Caf na kutupatia leseni za kutuhusu kuwatumia ni wachezaji ambao Gor Mahia haiwafahamu wao wataingia uwanjani wakiamini tutatumia kikosi tulichokitumia Kenya,” alisema Zahera.
Kikosi kinachotarajiwa kuanza ni; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Vicent Andrew ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Makapu, Pius Busitwa, Raphael Daudi, Matheo, Kaseke na Juma Mahadhi.
Kikosi hicho hakinipi matumaini na pia kutokana na matayarisho yasiyoridhisha na bila ya kupata mechi za kujipima na huku tukiona wengi wa kutegemewa hawamo basi sijui mgomo baridi, machofu au kutokuwa fiti. Ajib na Tambwe Yondani wakowapi?
ReplyDeleteKLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..
ReplyDeleteHusein Nyika maisha yake hatarini!!!
ReplyDelete