July 7, 2018


Mshauri wa timu za vijana nchini, Kim Poulsen, ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumlipa stahiki zake ikiwemo mshahara.

Taarifa zimeeleza Poulsen amekuwa akifanya kazi hiyo lakini amekosa mshahara kwa miezi kadhaa hivyo kupelekea kuamua kuandika barua kuomba kuachia ngazi ili kuwapa nafasi watu wengine.

Mbali na kutolipwa mshahara, imeelezwa pia Poulsen alipunguziwa mshahara katika utawala huu wa sasa tofauti na aliokuwa akipewa wakati wa Jamal Malinzi hivyo nayo inatajwa kama sababu mojawapo ya yeye kujizulu.

Kutokana na kujizulu kwa Poulsen, nafasi yake kwa sasa ipo wazi hivyo itabidi atafutwe mbadala mwingine ili kuziba pengo lake kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana hapa nchini.


5 COMMENTS:

  1. Labda huyo mwengine hatojali kufanya kazi bila ya malipo kwa moyo wa kujitolea

    ReplyDelete
  2. Katika hii kesi inayowakabili viongozi wa zamani wa TFF tumeona jinsi watendaji wa TFF walivyoongezewa mishahara mipya mara baada ya uongozi mpya kuingia mahakamani lakini mtu muhimu anapunguziwa mshahara lakini sio tu anapunguziwa hata kulipwa halipwi pia juzijuzi tumesikia tff wanadaiwa na kampuni ya ulinzi tatizo ni mfumo wetu wa kuchagua viongozi wa TFF unarudisha watu wa aina ileile

    ReplyDelete
  3. Tumelogwa. Hata kama simkubali Poulsen kwa viwango vya ufundishaji, lakini mshahara ni haki ya mtu lazima alipwe. Lipo tatizo la watendaji TFF kudhani kumlipa mtu mshahara ni fadhila hapana hiyo ni haki yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic