July 29, 2018


Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi Yanga nchini, Bakili Makele, ameibuka na kuja kitofauti zaidi kuhusiana na mchezo wa leo baina ya Yanga na Gor Mahia FC.

Mechi hiyo ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika itapigwa majira ya saa 1 jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo.

Makele ametamba kwa kusema kwa kikosi cha Yanga kilivyo sasa kuna uhakika mkubwa wa kupindua matokeo dhidi ya wapinzani wao ambao walishinda mechi ya mkondo wa kwanza jijini Nairobi.

Makele ameeleza kuwa ongezeko la wachezaji kadhaa kuelekea mechi hiyo ikiwemo Deus Kaseke, Mateo Anthony pamoja na Kelvin Yondani aliyeongeza mkataba wa miaka miwili utaleta chachu ya ushindi.

Aidha, kwa upande mwingine Makele amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga waje kwa wingi Uwanjani ili wamuone straika hatari mpya, Heritier Makambo, ambaye amesajiliwa kutoka Congo.

Makele amesema Makambo ndiye mbadala wa Donald Ngoma hivi sasa ambaye aliondoka Yanga kwa kuvunja mkataba wake na kuelekea Azam FC ya jijini Dar es Salaam.

Licha ya Bakele kuwataka Wanayanga kwenda kumshuhudia Makambo, mchezaji huyo hatokuwepo kwenye kikiso hicho kutokana na usajili wa jina lake CAF kuchelewa kusajiliwa.


2 COMMENTS:

  1. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete
  2. Wewe Bakili Makele usiwadanganye watu, hakuna cha Yondani au Makambo wote hao hawatacheza.....nyie kuweni wakweli lengo ni KUIDHALILISHA YANGA MWAKA MZIMA, KWA KUWA NA KIKOSI KIBOVU, UONGOZI WA UBABAISHAJI, NA USANII....ILI SIMBA WAENDELEE KUWACHEKA NA KUWADHIHAKI YANGA. HAKUNA mtanzania AMBAYE hajui kinachoendelea!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic