SIMBA YATOA TAMKO KUHUSIANA NA NIYONZIMA JUU YA KAMBI UTURUKI
Uongozi wa klabu ya Simba umefunguka kuhusiana na kiungo wake wake waliyemnyakua kutoka Yanga, Haruna Niyonzima juu ya kushindwa kuungana na wachezaji wenzake Uturuki.
Simba ipo jijini Instabul hivi sasa kwa kambi maalum ya wiki mbili ambapo inajiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na tamasha la Simba Day Agosti 8 mwaka huu.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa Niyonzima bado yupo kwao Rwanda kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kifamilia hivyo pindi atakapoyamaliza atarejea nchini.
Manara ameeleza kuwa mchezaji huyo kuna uwezekano mkubwa akarejea nchini kuanzia kesho Jumatatu na baadaye anaweza akasafiri kueleka Uturuki kujumuika na wenzake ambao wana takribani wiki moja sasa.
Ana damu ya Yanga huyo atawasumbua mpaka basi tehe tehe
ReplyDeleteNyie jishauen tu toka yupo Yanga huyu jamaa alkuwa na ttz hili hili La kupotelea kwao na sababu lukuki mliona mmepata eeh sasa zamu yenu
ReplyDeleteTatizo la Niyonzima ni hilo hilo miaka yote kujiona yupo juu na ni mchezaji muhimu kuliko wengine wote.
ReplyDeleteMara zote yeye ana matatizo ya kifamilia,asituletee dharau zake kama alivyokuwa Yanga,kama amekuja kufanya kazi na afanye kazi asituletee ujinga wake
Hili ni tatizo strategic camp inafanyika kwa mafungu
ReplyDeleteWho is Niyonzima by the way Simba is big brand in Africa now. Niyonzima take care brother you gonna lost very soon to come you are not above the club, you have to respect your employer
ReplyDeleteNamuonea huruma sana Simba inaviungo wengi wazuri zaidi yake.Haoni msimu uliopita watu wamechukua ubingwa bila hata ya kumjali. Sembuse msimu unao kuja? Team imekamilika sana anatakiwa aipigie magoti sio kama kule yanga alikokuwa juu ya wote.
ReplyDelete