KOCHA DJUMA AWAJIBU MASHABIKI SIMBA – VIDEO
BAADA ya klabu ya soka ya Simba kufungwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame jana usiku, kocha wa Simba, Masoud Djuma, amesema mashabiki hawatakiwi kulalamika kwa kutokuwepo baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Masoud ameyasema hayo kufuatia baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani kuonyesha kutoridhishwa na kiwango cha wachezaji waliopewa nafasi ambao wengi wao ni wale waliosajiliwa katika kipindi hiki cha usajili huku wachezaji wazoefu wakiachwa.
”Simba ina wachezaji 30, wengi wao wamecheza ligi na imeisha hawajapumzika, ikaja michuano ya SportPesa Super Cup kisha ikaja michuano hii ya CECAFA, mimi nikaamua wapumzike ili warudi kwenye ligi wakiwa vizuri na ninaamini itakuwa hivyo”, amesema.
Aidha ameongeza kuwa wachezaji wapya na wale ambao hawakupata nafasi kwenye ligi msimu uliopita ambao amewatumia kwenye michuano ya CECAFA, wameonyesha kiwango kikubwa na sasa anaweza kuamini ana kikosi kipana kwa ajili ya michuano mbalimbali msimu ujao.
Endapo Simba ingetwaa ubingwa jana ingekuwa ni mara yake ya saba kwani tayari ni mabingwa mara sita, wakishikilia rekodi ya kuchukua kombe hilo mara nyingi zaidi. Kwa upande wa Azam FC wao wametetea ubingwa wao ambao waliuchukua mwaka 2015 hivyo kuutwaa mara mbili.
Masoud Djuma ambaye ni raia wa Rwanda anaifundisha Simba kama kaimu kocha mkuu, baada ya aliyekuwa kocha mkuu, Pierre Lechantre, kumaliza mkataba na klabu hiyo mapema mwezi Juni na kurejea nyumbani kwao Ufaransa.
Wanaolalamika kwa Simba kutumia wachezaji tofauti kwenye kagame ni haki yao hii ni Tanzania ni nchi huru kutoa maoni hata kama yanakera lakini Simba kiukweli imelamba dume katika mashindano yale kuliko hata huyo Azam aliebeba kombe. Simba imefanikiwa kuwafanyia wachezaji viongozi wake waliokuwa wakijiuliza wapo vipi tathmini ya kutosha na kuona madhaifu yapo wapi. Tofauti na Azam ambao wametumia kikosi chao kamili kasoro labda Donarld Ngoma imempa simba faida ya taswira kamili ya kumjua mpinzani wake kikamilifu kuelekea ligi kuu. Wakati simba ikija kuunganika wachezaji wake wote na kuwa timu moja hakika itakuwa ni timu nyengine tofauti kabisa msimu unaokuja. Binafsi nawapa hongera sana wachezaji wale wa simba walioifikisha simba fainali kagame mwaka huu wamepambana na wanahitaji pongezi za kizungu maana wenzetu wazungu wao ni watu wa kuwapa moyo wachezaji hata iwe vipi kwakujua kuwa mara nyingi mchezaji anaumia zaidi kwa kutopata matokeo walioyataka.
ReplyDeleteMimi nawashangaa baadhi narudia neno BAADHI ya viongozi wetu wa Simba ambao wanachukia mashabiki wao kutoa maoni yao kuhusu timu yao. Tatizo lenu ni nini? Mnataka kusikia sifa tuu hamtaki mnapopewa mrejesho wa maoni ili kurekebisha kasoro? Mashabiki wanapolalamika timu kufanya vibaya, wanayo maoni ya kutoa. Jukumu lenu ni kuwasikiliza kuchukua maoni yao, yaliyo mazuri yafanyieni kazi, yasiyo mazuri mnayatupilia mbali. Shida iko wapi? Uongozi ni kuwasikiliza unaowaongoza. Waelezeni vizuri mashabiki wenu kwanini mnachukua hatua fulani, faida zake nini kwa klabu, mashabiki wataelewa, hakuna shida. Nawashangaa baadhi ya viongozi hawataki kusikia shabiki akitoa maoni kuhusu timu badala yake povu linawatoka. Mashabiki duniani kote kwenye mpira wana mchango mkubwa sana na wanaheshimika. Ni vizuri kuvumiliana badala ya kutoleana mapovu. Wote timu yetu moja.
ReplyDeletePOngezi nyingi sana kwa Kocha Djuma na wachezaji wa Simba wote kwenye Kagame. Narudia kusema BAADHI ya viongozi wala msikasirike mashabiki wa Simba kuhoji masuala ya timu yao. Ni haki yao ni upendo wao kwa timu, badala yake fanyeni kazi yenu ya kuongoza na pia waelimisheni na kuwapa taarifa thabiti mara kwa mara, msiwatolee povu, hiyo si sawa.
Delete