July 6, 2018


Wakati huohuo, Facebook iko katika mazungumzo na Ronaldo kuhusu kipindi cha runinga cha sehemu 13 chenye thamani ya $10m(Variety)

Masharti ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuhamia katika klabu ya Juventus yalikubaliwa wakati wa mkutano kati ya rais wa Real Florentino Perez , naibu wake Jose Angel Sanchez na ajenti wa Ronaldo Jorge Mendes siku ya Jumatano usiku. (Marca)

West Ham inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere , ambaye yuko huru baada ya kuondoka Arsenal.

Klabu hiyo imempatia kiungo huyo mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £100,000 kwa wiki (Sun)

Manchester City inakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Itali Jorginho, 26, baada ya Napoli kuthibitisha kuwasili kwa mchezaji atakayechukua mahala pake Fabian Ruiz, 22. (Manchester Evening News)

Beki wa Manchester City Aymeric Laporte, 24, anataka kuichezea Uhispania baada ya kuwachwa nje ya kikosi cha Ufaransa katika kikosi cha kombe la dunia (Manchester Evening News)

Manchester United iko tayari kumpatia kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 25, kandarasi mpya licha ya kuwekai mkataba wa miaka minne mnamo mwezi Aprili. (Sun)

Paris St-Germain inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Chelsea N'Golo Kante msimu huu.


Chelsea inataka dau la £100m kwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 lakini pia imemuorodhesha mchezaji wa Lyon mwenye umri wa miaka 21 Tanguy Ndombele, 21, kuchukua mahala pake (Goal)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic