July 24, 2018



Kikosi cha Simba kitaendelea na mazoezi yake kujiandaa na msimu mpya, leo.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wako nchini Uturuki kuendelea kujiandaa na msimu mpya wa 2018/19.
Ratiba ya Kocha Patrick Aussems raia wa Ubeligiji inaonyesha Simba itaendelea kupasha leo huku akiendelea kuongeza aina tofauti ya mazoezi.

Simba imekuwa ikiendelea na mazoezi na leo itakuwa ni siku ya tatu timu hiyo ikiendelea kujifua katika milima ya Kartepe nchini Uturuki.

2 COMMENTS:

  1. Ni wakati wa MO Ibrahim maana soka lake ni la Kibelgiji

    ReplyDelete
  2. Mo Ibrahim atakuwa anasumbuliwa na matatizo binafsi labda mwili wake ulikuwa haupo kamili asilimia mia moja kutokana na injury kwa hivyo alikuwa bado ana usikilizia na kama atakuwa fiti basi uwezo anao na anaweza kuleta ushindani pale Simba hata Boko na Okwi wanaweza wakasubiri. Lakini kama Mo Ibrahim hana tatizo la kiafya labda ni matatizo ya mawazo basi anatakiwa kubadilika haraka hasa ujio huu wa kocha mpya anatakiwa kumuimpress kocha huyu ili amuamini asije akafanya makosa kama yale yaliotokea kwa kocha alieondoka Lechant. Wazungu ni watu wenye kuamini sana usemi usemao the first impression is the last impression.. yaani muenekano wa mtu kitabia unapokutana nae kwa mara ya kwanza mara nyingi huwa ndio tabia halisi ya mtu huyo. Watanzania wengi tunaofuatilia soka huwa tuna sisitiza vijana wetu waijenge mii yao iwe imara lakini kwa bahati kabisa Mo Ibrahim na Mzamiru Yasini ni vijana waliojaiwa miili ya kazi licha yakuwa na vimo vya wastani. Kinachotakiwa ni koikomaza zaidi miili yao kimazoezi. MO anatakiwa kutafuta kanda za Mohamedi Husein aka Mmachinga atajifunza mengi kutoka kwake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic