July 24, 2018


Wakati straika hatari kutoka Azam FC, Shaban Idd Chilunda akitarajiwa kukwea pipa siku kadhaa zijazo kuelekea Spain, mshambuliaji mwingine kinda, Yahya Zayd, ameondoka jana kuelekea Afrika Kusini.

Zayd ambaye amekuwa katika fomu haswa msimu uliopita wa 2017/18 ameondoka kulekea nchini humo kwa ajili ya majaribio na Bidvest Wits inayoshiriki Ligi Kuu.



Kuna uwezekano Azam wakatwaa mpunga endapo Zayd atafuzu majaribio hayo kutokana na kuwa na mkataba na watengeneza koni hao wa Chamazi.

Ikumbukwe Zayd alisaini mkataba mwingine na Azam FC baada ya msimu uliopita kumalizika na sasa itabidi wamuuze kwa Bidvest Wits endapo watafurahishwa na majaribio yake.

Zayd atakuwa ataungana na beki aliyewahi kuichezea Simba endapo atafaulu majaribio, Abdi Banda ambaye kwa sasa anaichezea Baroka FC ambayo pia inashiriki Ligi Kuu nchini humo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic