July 24, 2018


Licha ya kumalizana vizuri na mabosi wa Yanga juzi, unaambiwa hali pale Jangwani si nzuri kutokana na mpango wa kukipeleka kikosi kuweka kambi Morogoro kukwama.

Katika kikao walichokaa juzi viongozi wa Yanga pamoja na wachezaji wa timu hiyo kilikuwa na lengo la kujadili juu ya mgomo baridi ambao umekuwa ukifanywa na wachezaji wakidai stahiki zao.

Safari ya kuelekea Morogoro ambayo ilipasw kufanyika jana ilikwama tena na badala yake programu ya kuendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi ikaendelea japo wachezaji baadhi wakigoma kwenda kushiriki mazoezi hayo.

Nyota aliyesajiliwa kutoka Simba kuelekea msimu wa 2017/18, Ibrahim Ajibu alikuwa miongoni mwa ambao hawakufika kwenye mazoezi hayo majira ya asubuhi.

Wachezaji wengine ni beki Hassan Kessy, kipa Beno Kakolanya, Andrew Vincent pamoja na Kelvin Yondani ambaye alitegemwa kuhudhuria mazoezi hayo baada ya kukutana na Abbas Tarimba siku kadhaa zilizopita.

Haijajulikana kama safari hiyo itakuwepo tena au la kutokana na mgomo huo ambao wachezaji wamekuwa wakiuendeleza ambapo walipaswa kuondoka jana kuelekea Morogoro kwa ajili ya kambi maalum kujiwinda dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa jijini Dar es Salaam, Julai 29 2018.

4 COMMENTS:

  1. Huna taarifa sahihi ndio maana umeshindwa kuandika kitu cha moja kwa moja. Safari kukwama na mgomo vitu viwili tofauti. Kama wachezaji kutokwenda mazoezini hao wachache kunaweza kusababisha safari kufa basi hata hao watatu wanaokwenda Uturuki wangesema wamegoma

    ReplyDelete
  2. Yanayotokea Yanga; yanaweza kutokea Simba endapo vichwa vinavyoendesha soka vitaendelea kuwa hivi hivi vya Mzee Akilimani na wajanja wachache wa mjini.

    ReplyDelete
  3. Maneno hayo si ya kuikwamua Yanga, hoja kushindwa kuondoka ziainishwe sababu tujue jinsi ya kushauri si kubahatisha hoja. Kwani viongozi wamesemaje?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic