July 26, 2018


Na George Mganga

Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa, amesema katiba ya Simba iliyosajiliwa mwaka huu 2018 baada ya mapendekezo kutoka kwa wanachama ndiyo itakayotumika katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa Radio One, Mkwawa amesema katiba mpya ya Simba iliyosajiliwa siku chache zilizopita imefuata taratibu zote mpaka serikali ikaamua kuipitisha ndiyo itakayotumika kwenye uchaguzi na si vinginevyo.

"Simba wameshakamilisha usajili wa katiba mpya ambayo imefuata taratibu zote, hivyo itakayotumika kwenye uchaguzi ujao ni hii ya 2018 na si vinginevyo" alisema.

Katiba hiyo ilifanyiwa mabadiliko kutoka ile ya zamani ya mwaka 2014 iliyokuwa inamtaka mgombea Urais kuwa na kiwango cha elimu ya kidato cha nne lakini hii ya sasa inamtaka awe na shahada ama digrii.

Simba walifanya mabadiliko hayo ambayo yaliyokuwa ni mahususi kwa ajili ya kuupokea mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo ambayo tajiri kijana, bilionea Mohammed Dewji Mo, amewekeza hisa zenye thamani ya bilioni 20.

Simba inatarajia kukutana Julai 31 kwa ajili ya kuanza mchakato mzima wa kumpata Rais mpya wa klabu hiyo ambaye ambaye atakuwa madarakani kwa miaka minne ijayo.

Kwa sasa Simba inaongozwa na Kaimu Rais, Salim Abdallah 'Try Again' kutokana na Rais wake, Evans Aveva kuwa mahakami kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha.

4 COMMENTS:

  1. Anayelinda usalama wa nyumba na heshima yake, si mwengine ila mwenye nyumba ambaye yeye ndie mwenye kugharimia aila ya nyumba hiyo na usalama wa nyumba hiyo kwakuwa yeye ndie alieijenga na ndie wakuionea uchungu. Mwenye nyumba hawezi kukaa pembeni akawaachia wengine wafanye watakayo wao kwasababu. Kuhusu uchaguzi unaonngojewa kwa hamu wa club ya simba hakuna mwengine wa kuiongoza kwa ursisi isipokuwa Mo yeye mwenyewe na hakuna ataelipinga hilo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sidhani kama Mo atakuwa kwenye nafasi ya kutaka kuwa mwenyekiti wa Simba..
      Kwenye ulimwengu wa soka la mafanikio yeye kawekeza pesa zake anatakiwa akae pembeni.. Akiwa pembeni itakuwa rahisi zaidi kwa yeye kuukosoa, kuuelekeza, kuukoromea na kuubana uongozi wa Simba ili kuleta mafanikio chana..

      Ila akijiingiza kwenye abdakadabra za uongozi wa soka na vilabu vyetu si muda mrefu tutaiona Simba ikianza kuvutana wenyewe kwa wenyewe..!!
      Kumbuka kuwa wapenzi, wanachama na wafuasi wa Simba wanataka ushindi hata palipo pagumu kushinda..! Hawataona shida kukomromea mwekezaji kisa tu timu imeboronga mechi 2,3..

      Ila i hope ipo siku tutafikia hatua ya kuwa na viongozi wa kuajiriwa kwa mikataba ya muda maalumu badala ya hawa wa kupigiwa kura kushika hatamu.!

      Delete
  2. Nafikiri ni vyema tukaelimishwa juu ya mfumo wa kiuongozi kutokana na katiba mpya ya simba. Tujue nyadhifa za kuchaguliwa na wanachama na nyadhifa za kutoka kwa mwekezji. Nafikiri kwa mujibu wa katiba mpya lazima sehemu zote mbili zitoe viongozi

    ReplyDelete
  3. Ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa Katiba mpya, kutaundwa Kampuni mbili ambazo ni Simba Sports Club Consolidated...ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia shares za wanachama wa Simba na pia itaundwa Simba Sports Club Company Ltd ambayo ndio itakuwa kampuni inayosimamia shughuli za kila siku za Club, huku sasa ndio kutakuwa na watendaji wa kuajiliwa, Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi wa Fedha, Mkurugenzi wa Masoko, among others...hivyo uchaguzi nahisi utahusu ile Bodi wa wajumbe wanane wanaowawakilisha wanachama wa Simba ...mwenye inputs zaidi karibu...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic