July 26, 2018


Baadhi ya wanachama wa Yanga wamepinga kitendo cha Omary kaaya kuteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo.

Mwanachama anayejulikana kwa jina la Juma Magoma, amefunguka na kusema uongozi wa Yanga haukufuata taratibu sahihi kwa kumteua Kaaya kuchukua nafasi ya Boniface Mkwasa aliyejiuzulu kwasababu za kiafya.

Kwa mujibu wa Radio One, Magoma amesema kiongozi yoyote anayeshika nafasi hiyo ni lazima awe au aliwahi kuwa katika nafasi ya Kamati ya Utendaji jambo ambalo ameeleza kwa Kaaya haikuwa hivyo.

Mwanachama huyo amedai Yanga hawajafanya uteuzi sahihi na ameshangazwa na maamuzi hayo ya kuteuliwa kwake kwani ni kinyume na taratibu.

Aidha, Magoma ameshangazwa na TFF kulipokea suala hilo bila ya kuhoji imekuwaje mpaka akateuliwa akidai kutakuwa na namna ya kujuana.

Magoma amesema TFF na Yanga watakuwa wanajuana kwani uteuzi wa Kaaya haukupaswa kufanyika kwasababu hajawahi kuwa kwenye Kamati ya Utendaji Yanga.

6 COMMENTS:

  1. Kwani katibu si muajiliwa au vipi. Huyu magoma yeye kila siku kupinga tu na kundi lake miaka mingi ana msaada wowote kazi kupinga tu

    ReplyDelete
  2. Navyofahamu kwa mujibu wa sheria ya club licencing ,katibu mkuu,afisa habari na mhasibu wanakuwa waajiriwa sio lazima watoke kwenye kamati. Hawa waandishi wanao wapa platform ndio wanawapa ujeuri,ange msomea sheria na kumalizana naye off air.

    ReplyDelete
  3. Chizi huyo anayepinga kwani mkwasa alivyoteuliwa alikua kwenye kamati ya itendaji au alikua anataka ateuliwe yeye?

    ReplyDelete
  4. Tumekusikia baba hata kama unasema utumbo ( usilojua ) ndio kawaida ya mtu mjinga hataki kuuliza ili ajulishwe maana.Katibu ni kazi ya kuaajiliwa sio ya kuteuliwa.

    ReplyDelete
  5. Wanaanza tena ukorofi wao, mtunzeni Amisi Tambwe huenda akasaidia tena kwa bao lake la mkono kama alivofanya kabla

    ReplyDelete
  6. Hivi nyie Waandishi kwa nn hamfati ethics za kazi zenu..Kwa nn inaruhusu utumbo kama huu?why msihoji hicho kifungu?Lini Mkwasa alikuwa kwenye kamati ya utendaji,hamjui waliopo kwenye Secretarieti ni waajiliWa?shame upon you

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic