NDEMLA BADO MWEKUNDU, AONGEZA MIAKA MIWILI SIMBA
Wakati kiungo Said Ndemla akiwa angani hivi sasa akielekea Uturuki kwa ajili ya kuungana na kikosi cha Simba, imefahamika ameshamalizana na mabosi wake kwa kuongeza mkataba wa miaka miwili.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu na ikiwa sababu iliyoelezwa kushindwa kuondoka pamoja na wenzake kwenda Uturuki Jumapili iliyopita.
Ndemla na Simba wamefikia makubaliano ya kuingia kandarasi hiyo baada ya kuchuka muda mrefu ambapo sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Ndemla yuko angani hivi sasa akiwa sambamba na Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga kwa ajili ya kambi hiyo ya wiki mbili ambayo Simba imeweka huko Instanbul, Uturuki.
Awali kulikuwa na tetesi za kuwa anataka kutimkia Sweden kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa lakini imeshindikana tena baada ya kuongeza miaka hiyo miwili.
Kikosi cha Simba kipo huko kujiandaa na tamasha la Simba Day pamoja na msimu mpya wa ligi huku kikitarajia kuanza safari ya kurejea nchini Agosti 4 2018.







Anaacha kwenda Ulaya kucheza professional football umri nao unakwenda!
ReplyDeleteHahahaa Yanga majeruhi walidai wamemzuwia kwenda Uturuki kwakuwa wamempa dau ati alishindwa Mo kumpa. Wajitutumuwa wasiambiwe wamekwisha
ReplyDeleteSi alisemekana amemalizana na Simba Muda na wamempa ruhusa kwenda Sweden ili ndio soka la bongo
ReplyDeleteMtapata tabu sana Yanga.Wasubirini kina Yondani, kessy wawatie changa la macho.
ReplyDelete