Katika kipindi hiki cha tetesi za usajili na usajili wa wachezaji katika ligi kubwa za Ulaya, kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza kuonyesha mechi za maandalizi ya Msimu mpya kwa ligi kubwa za barani ulaya. Mechi hizo ambazo huchezwa chini ya mashindano yanayofahamika kama Kombe la Mabingwa wa Kimataifa yaani ICC.
Mechi hizo ambazo zimeanza kutimua vumbi wikiendi iliyopita zinashirikisha vilabu bora 18 kutoka ligi tano kubwa barani ulaya. Miongoni mwa timu hizo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund (Bundesliga), Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal (Premier League), PSG (League 1), Barcelona, Real Madrid (La Liga), AC Milan, Inter Milan na Juventus (Serie A). Katika mechi zilizopigwa wikiendi iliyopita Borussia Dortmund wameonyesha kiwango kizuri baada ya kuwafunga Manchester City 1-0 na kuwachapa Liverpool 3-1.
Wapenzi wa Soka nchini watapata nafasi ya kuishuhudia michuano hii kupitia chaneli ya World Football na Sports Premium katika king’amuzi cha StarTimes ambao wana haki za kipekee za kuonyesha michuano hii.
“Kama ulikuwa unajiuliza nini kinafata baada ya Kombe la Dunia basi majibu ni haya, Katika kuonyesha kwamba sisi ni wafalme wa Burudani, tunakuletea mechi kali za ICC, maarufu kama Pre-Season yaani mechi za kujiandaa na msimu mpya, ambapo utawaona wachezaji wakubwa kama Ronaldo akiwa na klabu yake mpya ya Juventus, Mahrez akiwa na Man City, Mo Salah, Mane, Messi na wengine wengi”. David Malisa, Meneja Masoko wa StarTimes.
“Mechi hizi za ICC ama Pre-Season zinapatikana kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee hakuna king’amuzi kingine kinachoonyesha mechi hizi. Mechi zote zitaonekana kwenye chaneli ya World Football na Sports Premium ambazo zipo katika kifurushi cha MAMBO kwa watumaji wa Antenna Tsh 13,000 tu kwa mwezi na kifurushi cha SMART kwa wateja wa Dish kwa Tsh 19,000 tu kwa mwezi”, aliongeza Malisa.
Mbali na kuonyesha michuano ya ICC StarTimes wameongeza chaneli 5 Mpya katika king’amuzi chake na zitaanza kuonekana mapema mwezi wa nane.
“Katika kujali mahitaji ya wateja wetu pendwa kabisa, tumeongeza chaneli 5 mpya zaidi ambazo zitaanza kuonekana katika king’amuzi chetu kuanzia tarehe moja mwezi wa nane, chaneli hizo ni EBONY LIFE ya Nigeria, EWTN, Discovery Family ambayo ina vipindi vingi vya kifamilia, na DW kwa ajili ya Habari, pia tumeirudisha chaneli ya TV Imaan. Mbali na chaneli mpya tumeihamisha chaneli ya Fox Sports kutoka kifurushi cha UHURU kwenda kifurushi cha MAMBO.
Taadifa njema zaidi ni kwamba chaneli ya WASAFI TV sasa inapatikana kwa wateja wetu wa Dish chaneli namba 333 kote nchini. Ni wakati wa kuikata kiu ya Burudani ndo maana tunasema Baki na Sisi, Burudni inaendelea”. Zamaradi Nzowa, Meneja wa kitengo cha Maudhui, StarTimes.
Kuhusu StarTimes
StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”







0 COMMENTS:
Post a Comment